TIME INANAFASI GANI KATIKA MAISHA YAKO?
TIME INANAFASI GANI KATIKA MAISHA YAKO? Salim Msangi, Time, nyakati ni kitu cha ajabu sana … tulipo ishia kwenye posti ya mwisho, itahitaji tujue kitu cha maajabu kinacho itwa ‘time’, bila kukijua hicho, hatuwezi kunyanyua mguu mmoja kwenda mbele. Time ni mada pana sana, huenda siku moja nikaja kuitiririsha hapa, lakini kwa leo nitaigusa kidogo kwa minajili ya mada yetu, ili tuweze kulijibu swali tulilo achana kwenye posti iliyo isha. Tumeona kuwa kile ambacho kinafikiwa na milango yetu ya fahamu ni pungufu kwa asilimia 99.99..., dhidi ya kile ambacho hakifikiwi na milango yetu ya fahamu kwenye ulimwengu wote. Ulimwengu wetu tunaugawanya sehemu kuu mbili, ulimwengu wa kiwiliwili, na ulimwengu wa roho. Asilimia 99.99 … % kwa lugha nyepesi tunaweza kuita ndiyo ulimwengu wa roho, na kilicho bakia ndiyo uliwengu wa kiwiliwili. Hivyo kitu kinacho itwa ‘time’ tunaweza kukigawa kwenye aina mbili hizi za ulimwengu, yaani ulimwengu wa kiwiliwil...