Posts

Showing posts from December, 2018

DC TARIME ANUSURU MAISHA YA ALIYEFANYIWA TOHARA KIENYEJI

Image
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga ameyanusuru maisha ya kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la  Mwita Marwa mkazi wa Kemakorere baada ya kudaiwa kufanyiwa tohara isiyo Salama. Mkuu huyo wa wilaya ametoa msaada huo baada ya kumkuta kijana huyo akiwa ameanguka barabarani bila ya kupatiwa msaada wowote na wananchi waliokuwepo katika eneo hilo. Mkuu huyo wa wilaya alikuwa njiani kuelekea Nyamongo katika ziara yake ya kikazi. Inadaiwa kuwa kijana huyo alifanyiwa tohara hiyo isiyo salama huko porini na kuvuja damu nyingi zilizopelekea kuishiwa nguvu.

UKWELI KUHUSU CHRISMAS NA TAREHE YA KUZALIWA YESU

Image
"KUNA MSEMO WA KISWAHILI UNAOSEMA, "MWANAFUNZI HAMPITI MWALIMU WAKE" Mwisho utajua kuwa kanisa katoliki ndilo baba wa theolojia na mafundisho yote ya imani za Ukristo. Katika hili nakaa kimya Nachukua mafundisho ya Mwl. wangu wa Maandiko Matakatifu Pd. Titus Amigu kama yalivyo na kuwapa katika maandalizi ya kusherekea Krismasi hii 2018. TAREHE YA KUZALIWA KWA KRISTO Nimeombwa nifafanue tarehe ya kuzaliwa Yesu Kristo kama ni kweli ni tarehe 25 Desemba au la. Lakini kwa ajili ya kuwekana sana nimeyagundua maswali mawili yanayoweza kufuata baada ya kujibu swali hili la msingi. Ndiposa nimeambatanisha majibu kwa maswali hayo ya nyongeza. Swali moja ni kwa nini tunaadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo kila mwaka na lingine ni Yesu alitungwa mimba lini. Nifuatilie. Nitaanza kujibu swali la kwa nini tunaadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo kila mwaka, kisha nitajibu swali la tarehe ya kuzaliwa Yesu Kriisto na kumalizia na swali la Yesu alitungwa mimba lini. Mpangilio huu unasa...