UYOGA CHAKULA KITAMU NA TIBA YA MARADHI.

UYOGA CHAKULA KITAMU NA TIBA YA MARADHI.

Uyoga ni  chakula, tena wanaokifahamu  vizuri wanakwambia  ni  chakula  kitamu. Mbali ya kuula , Uyoga UYOGA una faida nyingi kwa binadamu. Uyoga  kama  chakula  una tumika kwa  namna nyingi tofauti naunaliwa  karibu katika  kira sehemu  duniani. Wakati kwa AFRIKA, UYOGA unaonekana kwamba nichakula  cha  kawaida ,kwaULAYA na MASHARIKI MBALI (ASIA) ni chakula muhimu na cha gharama  kubwa. kwa leo nitaelezea uyoga aina chaza  (OYSTER MUSHROOM) Pleorotus  florida (PFM) – mweupe Pleorotus floridanus(PFST )-Kahawia na wa porini. Uyoga wa Pleorotus  florida (PFM) na Pleorotus Floridanus (PFST) ndio unaolimwa sasa katika mikoa ya mbeya, iringa, Ruvuma,  Morogoro, Rukwa,pwani DSM, Arusha ,Kilimanjaro ,NK. Watanzania naomba tuchangamkie  kilimo cha uyoga.

Kina faida nyingi. wengine wanaula katika saladi, wengine wanatumia kuongeza ladha katika mayai, nyama, mchuzi wa tambi, wengine wanatengeneza supu na matumizi mengine tofauti.

VIINI LISHE NA FAIDA ZA UYOGA KATIKA KULINDA AFYA YA MWANADAMU.

Siku  hizi watu  wengi zaidi wanakuwa makini sana na vyakula wanavyokula ilikulinda afya zao .Baadhi ya vyakula hususanif  vile vyenye LEHEMU ama mafuta mengi husababisha maradhi mbalimbali mwilini kama shinikizo  la damu na mengineyo. Uyoga unapotumiwa kwa chakula kamwe hauleti madhara  yoyote bali faida nyingi hazipatikani katika vyakula vingi tunavyotumia. Katika uyoga kuna kiasi cha kutosha  cha protini ,kabohaidreti  na nishati. Lehemu (cholesterol) ambayo husababisha shinikizo la damu  na mengineyo ambayo hupatikana katika aina mbalimbali za protini, haipo kabisa katika uyoga.

Kadhalika ni katika protini za uyoga pekee ambako hupatikana aina zote tisa (9) muhimu za amino asidi ambazo ni muhimu katika kila mlo wa binadamu. Milinganisho ya protini, kabohaidreti , na lehemu na nguvu kati ya UYOGA  na aina mbalimbali za nyama ni kama ifuatavyo . ASIDI ambazo ni muhimu katika kila mlo kamili wa mwanadamu .

Kadhalika uyoga una aina mbili za vitamini, zikiwemo Thiamine (vitamin b1) riboflavin (vitaminiB2) Ascorbic Acid (vitamin C) Pamoja na folic acid. Utumiaji wa mara kwa mara wa uyoga hutoa ulinzi wa kutosha dhidi ya magonjwa yanayosababishwa na ukosefu  wa vitamin mwilini (kama  vile Beriberi,Pellagra Na Scurvy).

Uyoga mkavu una viini lishe vifuatavyo (1) Protini 20% -45% (2) vitamini B,C,D,E,K,        (3) Madini Calcium, Phosphorus, Chuma, na kiasi kidogo cha mafuta na mengineyo .

TIBA: Husaidia kutibu/ kupunguza shinikizo la damu, kisukari , vidonda vya tumbo, saratani (kansa), Figo, moyo, uvimbe, vidonda vya mwili, kiungulia, vipara, fangasi aina zote, kifua kikuu, kuongeza kinga ya mwili na kuuwezesha kupigana na magonjwa mbalimbali, kuyeyusha na kusaga takataka zenye asili ya kaboni. Huongeza maziwa kwa akina mama wanaonyonyesha, saratani ya damu (Leukemia), Ini na mengineyo mengi.

Uyoga unafaa sana kwa waathirika wa UKIMWI.

Faida nyingine ya uyoga ni kusafisha mazingira kwa vile uyoga huoteshwa kwa kutumia mabaki yatokayo mashambani, viwandani na nyasi (majani ya maharagwe, mpunga, randa za mbao n.k). Kuotesha uyoga kwa kutumia takataka hizo ambazo zingekuwa kero kwa jamii ni njia mojawapo ya kusafisha mazingira na mabaki yakishatumika kuoteshea uyoga yanafaa sana kurutubisha ardhi (Mbolea).

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!