Posts

Showing posts from August, 2018

UTAFITI: NJUGU ZINAVYOBORESHA NGUVU ZA KIUME.

Image
Utafiti: Njugu zinavyoboresha nguvu za kiume   Moja kati ya changamoto kubwa inayoikabili dunia hivi sasa, ni tatizo la kuzorota kwa ufanisi katika utungaji mimba ili kufanikisha agizo la Mwenyezi Mungu, “Zaeni Mkaongezeke”. Tatizo hilo kwa asilimia kati ya 40 hadi 50, kwa mujibu wa tafiti za kisayansi linasababishwa na wanaume kutokuwa na mbegu bora zenye ufanisi ikiwa ni pamoja na tatizo la nguvu za kiume. Katika kutafuta suluhisho, mengi yamefanywa na watafiti na kubainika kuwa ulaji, unywaji na uvutaji ni chanzo kikuu cha tatizo hilo. Utafiti uliofanywa hivi karibuni na wanasayansi nchini Marekani umebaini kuwa njugu zinaweza kusadia kuboresha mbegu za kiume na kuongeza nguvu za kiume. Watafiti hao, katika kutafuta majibu ya matokeo ya njugu, liliwatumia wanaume 119 wenye umri kati ya miaka 18-35. Watafiti hao waliwagawa wanaume hao katika makundi mawili, kundi moja la wanaume walikula njugu gramu 60 kwa siku kwenye mlo wao. Halafu kundi lingine halikujumuisha njugu...

FAHAM AFYA YAKO KUTUMIA RANGI YA MKOJO

Image
FAHAM AFYA YAKO KUTUMIA RANGI YA MKOJO Je unafahamu ya kwamba rangi ya mkoja inakupa matokea sahihi kuhusu afya yako? Kama jibu ni hapana basi makala haya yanakusu wewe, kwani rangi ya mkoja kwa mujibu wa watalamu wa afya unauwezo mkubwa wa kukuoa ukweli juu ya afya yako. 1. Mweupe kabisa (Usio na Rangi): Unakunywa maji mengi. 2. Manjano iliyochanganyika na Kijani kidogo. Ni kawaida, una afya na Mwili wako una maji ya kutosha. 3. Manjano iliyo pauka.Upo kawaida tu. Endelea kunywa maji ya kutosha 4. Njano iliyo kolea. Upo kawaida lakini unashauriwa kunywa maji ya kutosha. 5. Njano inayokaribia kufanana na Kahawia au Rangi kama ya Asali. Mwili wako hauna maji ya kutosha. Kunywa maji kwa wingi sasa. 6. Rangi ya Kahawia. Huwenda una Matatizo kwenye Ini lako au Upungufu mkubwa wa Maji mwilini. Kunywa maji ya kutosha na umwone daktari kamali hii ikiendelea. 7. Rangi ya Pinki inayokaribia kuwa kama Nyekundu. Kama hujala matunda yoyote yenye asili ya uwekundu, basi huwenda una ...

FAHAM NJIA ZA KUEPUKA KUWA NA HARUFU MBAYA MDOMONI.

Image
FAHAM NJIA ZA KUEPUKA KUWA NA HARUFU MBAYA MDOMONI. Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla. Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni uondoa haiba ya kupendwa kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea moja kwa moja na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni mwako. Chakula unachokula kina athiri hewa inayotoka mdomoni au sehemu nyingine za mwili wako. Baadhi ya vyakula vina matokeo mabaya sana kwa hurufu unayotoa mdomoni.  Harufu mbaya mdomoni si ugonjwa wa kuambukiza haina haja kuogopa ukikutana na mtu mwenye harufu mbaya mdomoni kwamba atakuambukiza. Pia tatizo kubwa ni kwamba watu wenye harufu mbaya mdomoni hawajijui kwamba wana harufu mbaya. Asilimia 85 - 90% ya tatizo la harufu mbaya mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi). Harufu nyingi mbaya mdomoni hutokana na vyakula vyenye asilia y...
Image
WANAUME, NA WANAWAKE, HIZI NDIZO ISHARA KUWA BINTI HUYO HANA NIA YA KUINGIA KATIKA UHUSIANO WA MUDA MREFU NAWE. Mwanamume mmoja aliwaandikia wanaume wenzake tahadhari kuhusiana na ikiwa msichana alikuwa na nia ya kukaa kwa muda mrefu au kutoweka baada ya muda mfupi. Ishara kwamba hataki uhusiano wa kudumu Zifuatazo ni pointi alizotoa kutetea wazo lake. Wanaume mnaweza kusoma kutoka kwake ikiwa hamtaki kuvunjika moyo. 1. Anakuweka siri? Ikiwa hajawajulisha marafiki wake au dada na ndugu zake kukuhusu, huenda wewe siye anayetaka kutolea maisha yake. 2. Hayuko katika mipango yako ya siku za usoni? Ikiwa umemtajia mipango yako unayotaka kumshirikisha na umegundua hana hamu katika mipango hiyo, ni wazi kabisa unapoteza muda wako. 3. Mawasiliano Ishara kwamba hataki uhusiano wa kudumu Ikiwa mawasiliano kati yenu yameadimika, basi hakuna haja ya kuwa katika uhusiano huo. Picha: UGC Wanawake hudhaniwa kupenda sana kuzungumza. Lakini ukiona ameanza kuepuka mazungumzo nawe,...

FAHAMU SABABU ZA KUWA NA U.T.I SUGU

Image
FAHAMU SABABU ZA KUWA NA U.T.I SUGU MAAMBUKIZI kwenye njia ya mkojo ( Urinary Tract Infection kifupi U.T.I) ni maambukizi yanayoshika nafasi ya pili kuupata mwili mara nyingi zaidi. Maambukizi haya hufanya mtu kukosa raha na kwa baadhi ya watu hasa wanawake ni tatizo la kiafya linalojirudiarudia mara nyingi. Kwa bahati mbaya ni kwamba tiba iliyozoeleka kwa U.T.I ni kutumia dawa za kuua bakteria (antibiotics) ambapo bakteria wanaosababisha ugonjwa huu wanaoitwa E.coli wameanza kuwa sugu dhidi ya hizi dawa hivyo kusababisha wagonjwa wengie kupata U.T.I sugu. U.T.I ni mkusanyiko wa maambukizi eidha ya fangasi, virusi au bakteria ambayo yanatokewa kwenye njia ya mkojo ya mwanamke na mwanaume. Tunaposema njia ya mkojo tunaongelea figo zote mbili, mirija inayotoa mkojo kutoka kwenye figo hadi kwenye kibofu cha mkojo huitwa ureter, kibofu chenyewe  na mrija wa kutoa mkojo nje kutoka kwenye kibofu. Kazi ya figo ni kuchuja maji yaliyopo kwenye damu na kutoa maji yaliyozidi na taka...

Mama Kanumba ampigia magoti Muna kufuatia kauli yake ‘Muna alinitukana sana, Mungu ametenda’

Image
Mama Kanumba ampigia magoti Muna kufuatia kauli yake ‘Muna alinitukana sana, Mungu ametenda’ Mama Mzazi wa Marehemu Kanumba, amemuomba msamaha mwanadada Muna Love kutokana na maneno yake “Muna alinitukana sana, na mungu ametenda” kauli ambayo aliyatoa siku chache baada ya Muna kufiwa na mtoto wake. mama huyo alidai aliitoa kauli hiyo kwa hasira kwani mwanadada huyo wakati yeye amefiwa na mtoto wake Kanumba alizungumza maneno machafu juu yake. Akiongea na Time Fm wiki hii, Mama Kanumba alisema kwamba watu hawakumuelewa alichokimaanisha na watu walikata video fupu tu ya yale yaliyosambazwa. “Muna mwanangu pole sana, ni donda hilo ambalo haliponi ni donda ndugu ila naomba unisamehe Mama Kanumba amesema kwamba hana nia mbaya na hakuomba kitokee kilichotokea, watu walininukuu vibaya. Na wewe maneno uliyonisema mwanzoni hukujua kesho mwanangu, wote ni mapenzi ya mungu mimi sina nia mbaya,” alisema Mama Kanumba. Mama Kanumba amesema kwamba hana nia mbaya na hakuomba k...

CHINA YAONYA NCHI YEYOTE YA KIGENI KUINGILIA MASWALA YA CAMBODIA

Image
CHINA YAONYA NCHI YEYOTE YA KIGENI KUINGILIA MASWALA YA CAMBODIA. Afisa mwandamizi wa China amempongeza Waziri Mkuu wa Cambodia Hun Sen kwa ushindi wa chama chake katika uchaguzi wa wabunge wa Jumapili. Wakati huo huo imeonya nchi yoyote kuingilia uchaguzi huo baada ya upinzani kudai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu mkubwa, huku nchi za magharibi zikiendelea kukosoa utawala wa nchi hiyo. China ni mshirika mkuu wa kiuchumi na kidiplomasia wa Cambodia. Chama cha CCP kinachoongozwa na Hun Sen, aliyekuwa askari wa Khmer Rouge, kilitangaza kuwa kilishinda viti 125 katika uchaguzi wa wabunge, uchaguzi ambao chama kikuu cha upinzani cha PSNC hakikushiriki baada ya kuvunjwa mwaka uliyopita. Naibu kiongozi wa PSNC alitaja uchaguzi huo kama "kifo cha demokrasia". Mjumbe wa serikali ya China Wang Yi, mwanadiplomasia wa juu katika nchi hiyo, amesema katika taarifa kwamba uchaguzi ulikuwa ni udhihirisho katika "kuunga mkono" na "kuwa na imani...

Karibu katika asubuhi kuangalia vichwa vya habari katika magazeti ya Leo August, 2

Image