WANAUME, NA WANAWAKE, HIZI NDIZO ISHARA KUWA BINTI HUYO HANA NIA YA KUINGIA KATIKA UHUSIANO WA MUDA MREFU NAWE.

Mwanamume mmoja aliwaandikia wanaume wenzake tahadhari kuhusiana na ikiwa msichana alikuwa na nia ya kukaa kwa muda mrefu au kutoweka baada ya muda mfupi.

Ishara kwamba hataki uhusiano wa kudumu

Zifuatazo ni pointi alizotoa kutetea wazo lake. Wanaume mnaweza kusoma kutoka kwake ikiwa hamtaki kuvunjika moyo.

1. Anakuweka siri?

Ikiwa hajawajulisha marafiki wake au dada na ndugu zake kukuhusu, huenda wewe siye anayetaka kutolea maisha yake.

2. Hayuko katika mipango yako ya siku za usoni?

Ikiwa umemtajia mipango yako unayotaka kumshirikisha na umegundua hana hamu katika mipango hiyo, ni wazi kabisa unapoteza muda wako.

3. Mawasiliano

Ishara kwamba hataki uhusiano wa kudumu
Ikiwa mawasiliano kati yenu yameadimika, basi hakuna haja ya kuwa katika uhusiano huo. Picha: UGC
Wanawake hudhaniwa kupenda sana kuzungumza. Lakini ukiona ameanza kuepuka mazungumzo nawe, jua kuwa chuma chako ki motoni.

4. Anapenda uhuru wake sana?

Ikiwa mwanamke ataona vyema kujiendesha wakati wa mkutano wako na yeye, au hatakuomba msaada wa aina yoyote licha ya kuwa na hitaji au anasikia uchungu akikuona kwa nyumba yake ingawa mmekuwa mkishiriki mapenzi kwa mwezi, basi, unahitaji kujishughulisha, hana haja na wewe.

5. Hajakukwamilia?

Unahitaji kuwa na hofu ikiwa amekupa uhuru wote wa kujiburudisha na kusherehekea na marafiki wa kike au kiume unavyotaka.

Ikiwa hajalishwi na hilo, kuna shida, tafuta njia ya kuondoka mapema kabla ya kuumizwa moyo.

6. Anapenda sana maisha yake?

Ishara kwamba hataki uhusiano wa kudumu
Ikiwa anapenda maisha yake, basi unahitaji kuwaza aina ya uhusiano wenu. Picha: UGC
Ikiwa mwanamke hajali uhusiano wenu au mapenzi baina yenu na amejipa shughuli maishani, hauhitaji kuambiwa na mtu kuwa ni wakati wa kuondoka, fanya hima.

7. Hataki kuzungumzia maswala muhimu?

Ikiwa haonekani kuchukulia kwa uzito mazungumzo muhimu unayoanzisha na anakupa vijisababu, ni wakati wako wa kuondoka, hakutaki kwa uhusiano wa kudumu.

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!