Nyayo za wageni kutoka sayari ya mbali zagundulika No.3




HISABATI

Wagiriki walipokuwa wakirikodi tarakimu, hawakuweza kuzidi ’10,000’ kilichozidi hapo kwa wagiriki kilirikodiwa sawa na ‘infinity’, yaani kisicho na mwisho.

Ajabu ni kuwa watu walio ishi Syria ya kale, milenia kadhaa kabla ya Wagiriki walirikodi nambari zenye tarakimu kumi na tano! Hata kompyuta haiwezi kurikodi tarakimu kumi na tano! Hawa watu si walikuwa mbali kushinda wagiriki, lakini mbali kutushinda sisi kwenye zama za sayansi na teknolojia? Who are they?

Peru walifahamu matumizi ya ‘sifuri’, 0 ni tarakimu muhimu katika mahesabu yoyote yale, bila hiyo hakuna haesabu inayofanyika, kompyuta na program zake zinajengwa kwenye msingi wa 0 na 1. Siyo Peru peke yake, India, Mexico, Babiloni, China kutaja kwa uchache.

Ni kweli Darwin alikuwa najua anacho kisema?

Hesabu za maumbo, hesabu za desimali, zilikuwa zinafahamika maelfu ya miaka hata kabla ya wale walio itwa ‘wavumbuzi’ wa hesabu hizo kuzaliwa! Mara nyingi wanao itwa ‘wavumbuzi’ unakuta ni watu walio tafsiri kazi hizo kutoka kwenye vyanzo vingine na hasa vya kale mno na kuleta kwenye lugha inayofahamika wakati huo, lakini hawasemi ni wapi wametolea kazi hizo.

Hakuna jipya chini ya Jua. Hesabu hizo zilifahamika Mexico, Egypty, Peru, Babilon, Ur, Chaldea.

Kipenyo cha ‘Great Pyramid’ la Gaza, Kairo, Misri na kipenyo cha ‘King Cahmber’ kilichomo ndani ya Piramidi vinahusisha pembe tatu ya ‘3 by 4 by 5 na 2 by 3. Aina hii ya pembe tatu ndiyo ile iliyotumiwa na mwana mahesabu wa Kigiriki Pythagoras ambaye kwa kufuata historia ya kiserikali aliishi miaka 2000 baada ya Pyramid kujengwa, na yeye eti anaitwa ‘muasisi’ wa hesabu hizo za pai. Lakini tukifuata historia ‘mpya’ isiyo na ukakasi ni kuwa mwana mahesabu huyo aliishi miaka 15,000 baada ya Piramidi hizo kujengwa. Niambie ni wapi Pythagoras ‘alivumbua’ hesabu hizo?


Ukija kwenye hesabu za ‘phi’, aljebra, trigonometry, squre roots, cube root, na Logarithims tunakuta jamii za kale mno kushinda hata hao wanao itwa ‘wavumbuzi’ wa hesabu hizo walikuwa wanazijua. Egypty, Mesopotamia, Ur, Babilon, India, Peru, China kutaja kwa uchache. Ni kama hizi kazi tunazikopi kutoka mahala fulani, ni kama kuna wateule fulani wanao teuliwa kupitia miiko na taratibu fulani ambao wanakwenda kujifundisha maarifa haya kwa siri ikisha baadae wanakuja kutuambia kuwa fulani, ‘kavumbua’ kitu fulani.


Egypty ya kale walikuwa na alama fulani ya kimahesabu waliyo itumia kuonesha ‘mamilioni’ yaani badala ya kila wakati kuandika tarakimu yenye masufuri mengi, walibuni alama ya kimahesabu ya kuonesha kitu hicho. Hilo linaweza kufanyika endapo kitu hicho kinayo matumizi ya mara kwa mara na hivyo kumrahisishia mtumiaji wake asipate tabu, kama vile ambavyo leo tunatumia, MB, GB, TB n.k.

 Lakini cha ajabu ni kuwa dhana ya mamilioni sisi tumeanza kuitumia kwenye karne ya 17, yaani juzi tu; sasa ni akina nani hao ambao walikuwa Egypty na katika zama zipi ambazo mamilioni kilikuwa kitu cha kawaida mno kiasi kuwekewa alama mahususi kumrahisishia mtumiaji?

Niendelee kukuchosha na ugonjwa wa taifa, a.k.a ‘Hisabati’?

Twende kwingine usije ukakimbia blogi yangu bure kwa kudhania nafundisha hisabati hapa....read more
      By....salim msangi

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

FREEMASON NA ALAMA ZA SIRI MIKONONI