Je, hivi unadhani kwamba tupo peke yetu katika ulimwengu mzima? HAPANA

Je, hivi unadhani kwamba tupo peke yetu katika ulimwengu mzima? HAPANA

Kuna bilioni mia ya nyota zilizopo angani ambazo nazo karibu zote huwa kama zimezunguka Sayari moja ambapo nyota hizo huwa ni panoja na Gesi na vumbi na mgandamizo wa uvutano uliopo angani kwa pamoja huitwa Galaxy. Ambapo njia moja ya maziwa ya Galaxy hiyo, Jua huzungukia kila miaka milioni 200.,

Sasa kuacha hiyo Galaxy moja kuna Galaxy nyingine ambayo ni Andromeda:
Ambayo hiyo nayo huwa Inasadikika na wanasayansi ya anga kuwa itachukua njia hiyo miaka bilioni kadhaa ijayo! Hata aliyetafiti sidhani kama atakuwepo! Andromeda hiyo pia hujulikana kama Messier 31, au NGC 224

ni galaxy ya juu takriban 780 kiloparsecs (miaka milioni 2.5 ya mwanga) kutoka Dunia, na galaxy kuu karibu na Milky Way. ] Jina lake linatokana na eneo la mbingu ambalo imetokea,

Kuachana na hiyo teyari zimeshaonekana katika Darubini za watafiti hao wanajua wenyewe na kusema zipo bilioni 100 hadi sasa lakini huenda picha inavyoonekana ni kwamba zinaweza kufika hadi bilioni 200 nakuendelea hawajui bado,

Katika hiyo njia ya maziwa inayobeba karibu Galaxy bilioni 200 na zaidi ni moja tu kati ya 100,000 ya njia za maziwa zilizopo kwenye mtandao wa njia za maziwa uliopo angani katika safari ya mwanga wa muda wa miaka zaidi ya bilioni 2 na sehemu ambapo mabilioni na mabilioni ya Galaxy huunganishwa katika njia hiyo ya maziwa ambazo ndio mkusanyo mzima baada ya kutokea kwa Big Bang ndio tunapata kuona kile kinachoitwa Ulimwengu.
Watu wengi hudhani ulimwengu ni dunia hapana. ulimwengu ni kila kitu kilichopo angani kwa ujumla wake.
Basi pale wanapokosa majibu wenye kutaka kujua kuhusu Aliens kuachana na Blah Blah za wazungu Hapa The Creator/The Source/The Owner of the Universe anawapa majibu kuhusu hilo wanaloliuliza kwamba:

Allah (Mwenyezi mungu) anasema katika Qur.an:

Aya ya 57 Sura Al Ghafir

لَخَلۡقُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ أَڪۡبَرُ مِنۡ خَلۡقِ ٱلنَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَڪۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

"Kwa hakika uumbwaji wa mbingu na ardhi ni mkubwa(mpana) Lakini wengi wa wanadamu hawafahamu hili"

Aya ya 8 sura An Nahl 16

وَيَخۡلُقُ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

"Na kaumba yale msiyoyajua,mambo ambayo hamta yajua".

Aya ya 29 sura Ash-shuraa 42

وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦ خَلۡقُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَثَّ فِيهِمَا مِن دَآبَّةٍ۬‌ۚ وَهُوَ عَلَىٰ جَمۡعِهِمۡ إِذَا يَشَآءُ قَدِيرٌ۬

"Na katika vitendo vyake ni uumbaji wa mbingu na ardhi, na kwa wanyama wowote aliyo yatawanya. Na anaweza kuwakusanya wakati atakavyo"

Na anaposema mbingu katika surat Yusuph tunapata tafsiri yake kwamba sio mbingu zetu tu tunazoziona bali ni kila kilichopo nje ya dunia hii tuliopo.

Hivyo unatakiwa uelewe ya kwamba mwenyezi mungu kaumba vingi tofauti na malaika majini na binadamu na vingine unavyoviskia na ambavyo hujawahi kuviskia wala kuviona hata kuvihisi. Na lau angelitaka basi vyote angeviweka pamoja na sehemu moja na akitaka atafanya hivyo that's why second life is still unknown until you reach there you find out yourself tunaweza tukahisi umefika kwa Muumba wako kumbe bado unakatiza tu Kariakoo au Nyegezi halafu huonekani,

lakini pia mwenyezi mungu anasema katika sura Al Isra aya ya 70

وَلَقَدۡ كَرَّمۡنَا بَنِىٓ ءَادَمَ وَحَمَلۡنَـٰهُمۡ فِى ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ وَرَزَقۡنَـٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ وَفَضَّلۡنَـٰهُمۡ عَلَىٰ ڪَثِيرٍ۬ مِّمَّنۡ خَلَقۡنَا تَفۡضِيلاً۬

"Kwa hakika tumewapa wana wa Adamu. Tunawachukua(wamewekwa) juu ya ardhi na baharini, na tumewapa mambo mema, na tukawachagua juu ya wengi tuliowaumba kwa viwango vyema".

Ambayo hapo utaona kuwa tumependelewa zaidi kuliko wao pia lakini tumependelewa vya juu lakini sio Juu kabisa,

Sasa katika kuumbwa huku katika ulimwengu huu tuliopo je ni kina nani wapo juu kabisa?

ni sisi, na je ni nani aliyetusujudia? ni Malaika na Majini, sasa leo duniani unazidiwa maarifa na shetani na akhera malaika wanakutesa? upo sawa?

Lakini kumbuka katika aya ya Al Isra kwamba tumepewa mengi na kupendelewa lakini sio yote.

Hivyo amini usiamini kuna ambao wamepewa zaidi ya sisi na lau kama mwenyezi mungu angetaka angetukutanisha pamoja sote na tungekuwa pamoja na hata akitaka hilo.
Na kwa aya hizo nadhani utaelewa kuwa kuna hivyo viumbe vingine tofauti na tunavyovijua lau kama Mungu akitaka basi atatuonyesha ndio maana Muislam akiona kitu chochote tofauti hutoa shahada na kumtukuza mwenyezi mungu

Rakims 

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!