Posts

Showing posts from April, 2018

Siasa na Mabepari.

Image
Mtoto mdogo alimfuata baba yake na kumuliza, "Nini maana ya SIASA?". Baba akajibu, "Mwanangu, ngoja nijaribu kujibu kwa mfano huu. Mimi natafuta fedha ya matumizi, hivyo niite mimi BEPARI, Mama yako yeye anasimamia matumizi ya fedha, hivyo mwite SERIKALI. Mimi na mama yako tuko kwa ajili ya kuwapa nyie mahitaji yenu, hivyo nyinyi twawaita WANANCHI. Dada wa kazi yeye anatusaidia kazi za hapa ndani hivyo tunamwita MFANYAKAZI. Na mdogo wako ambaye ni mdogo tumwite FURSA ZA BAADAYE. Haya sasa mwanangu hebu fikiri na uone kama ninakupa jibu la kuridhisha! Kijana akaondoka na kwenda kulala huku akifikiri na kuyatafakari maneno aliyoyasema baba. Baadae usiku ule, akasikia mtoto ambaye ni mdogo wake akiwa analia hivyo akaamua kuamka na kwenda kumcheki. Akaona mtoto kajinyea na kajipaka uchafu huo huku akilia kuashiria anahitaji msaada. Akaamua aende chumbani kwa baba na mama, akamshuhudia mama akiwa peke yake kalala usingizi mzito na hana habari yoyote....

HUWA NAIPENDA SANA KUISOMA HII , LEO NGOJA NISHEE NANYII

Image
HUWA NAIPENDA SANA KUISOMA HII , LEO NGOJA NISHEE NANYII SOMA HII STORY UNAWEZA UKAJIFUNZA KITU. Kijana mmoja alisafiri kwa meli na rafiki zake, wakiwa katikati ya safari yao meli ilianza kuzama. Watu wengi pamoja na rafiki wa yule kijana walikufa maji wakati wanajaribu kujiokoa kwa kuogelea, lakini yule kijana alifanikiwa kushika ubao ulioelea majini akaanza kuelea nao, maji yalimpeleka hadi kisiwa cha mbali sana ambako hakukuwa na watu wala wanyama isipokuwa wadudu tu! Alifika ufukweni amechoka sana na asiyeamini tukio lililotokea, akaishi huko kwa kula matunda. Aliweza kujenga ka-kibanda kwa shida sana maana hakuwa na shoka wala panga, hatimaye akaanza maisha mapya. Aliishi muda mrefu kisiwani na tayari alishazoea mazingira yale ya shida japo shida haizoeleki. Mara zote nyakati za jioni aliwasha moto kwa kupekecha vijiti. Siku moja kama kawaida yake aliwasha moto nje karibu na kibanda chake, aliota moto muda mrefu hatimaye akapitiwa na usingizi. Alilala hapo hap...

SOMA HII STORY UNAWEZA UKAJIFUNZA KITU.

Image
SOMA HII STORY UNAWEZA UKAJIFUNZA KITU. Kijana mmoja alisafiri kwa meli na rafiki zake, wakiwa katikati ya safari yao meli ilianza kuzama. Watu wengi pamoja na rafiki wa yule kijana walikufa maji wakati wanajaribu kujiokoa kwa kuogelea, lakini yule kijana alifanikiwa kushika ubao ulioelea majini akaanza kuelea nao, maji yalimpeleka hadi kisiwa cha mbali sana ambako hakukuwa na watu wala wanyama isipokuwa wadudu tu! Alifika ufukweni amechoka sana na asiyeamini tukio lililotokea, akaishi huko kwa kula matunda. Aliweza kujenga ka-kibanda kwa shida sana maana hakuwa na shoka wala panga, hatimaye akaanza maisha mapya. Aliishi muda mrefu kisiwani na tayari alishazoea mazingira yale ya shida japo shida haizoeleki. Mara zote nyakati za jioni aliwasha moto kwa kupekecha vijiti. Siku moja kama kawaida yake aliwasha moto nje karibu na kibanda chake, aliota moto muda mrefu hatimaye akapitiwa na usingizi. Alilala hapo hapo hadi usiku wa manane aliposhtushwa na joto kali lisilo ...

FAHAM TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Image
FAHAM TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME Nguvu za kiume: Huu ni uwezo wa mwanaume katika kustahimili kufanya tendo la ndoa. FAIDA ZA TENDO LA NDOA. i) Huongeza kinga za mwili; huongeza nguvu ya kinga ya mwili(Immunoglobin A) hivyo husaidia kutougua magonjwa mbali mbali. ii) Huimarisha afya ya moyo; hupunguza ugonjwa wa moyo kwa 45% kwa wanaofanya walau Mara 6 kwa mwezi kuliko wanaofanya Mara moja kwa mwezi na pia hupata faida ya mazoezi na kuleta uwiano sawa wa testosterone na estrogen ambazo ni muhim kwa afya ya homoni ya mwanaume na ya moyo na mishipa ya dam(Cardiovascular system) iii) Hupunguza msongo wa mawazo, shinikizo la damu(Presha ya kupanda au kushuka), na kuboresha misuli ya mgongo,kiuno,kifua hivyo ni zoezi tosha. iv) Hupunguza maumivu; Hisia nzuri za tendo la ndoa huzalisha homoni zinazosaidia kupunguza maumivu ya miguu, mgongo, sehem za maungio na kichwa. V) Huzuia Saratani ya Tezi Dume, kwa kumwaga shahawa Mara 21 kwa mwezi yaani Mara 5 kwa week nikimaanisha kuf...

SIMULIZI; MAMA KAENDA KUPUMZIKA MIMI NIMEBAKI KUKULINDA

Image
SIMULIZI; MAMA KAENDA KUPUMZIKA MIMI NIMEBAKI KUKULINDA Juzi nilihudhuria msiba wa rafiki yangu mmoja na mkewe. Yeye na mkewe walifariki kwa ajali ya gari, wameacha watoto wawili mmoja wa miaka kumi na mwingine wa miaka minne wakike, mkubwa ni wakiume. Sasa tukiwa kwenye ule msiba, mimi kama rafiki nilikua karibu sana na wale watoto kwani wananifahamu kama Baba mdogo, kusema kweli nilichokishuhuduia kilinifanya nije nimpende mke wangu mara mia zaidi. Kweli nampenda sana mke wangu lakini kuna wakati namchukuliaga poa nikiwa na mambo yangu najifanya kidume na namuudhi. Kwasiku tatu zote nilikua karibu na ile familia tukimalizia msiba, katika kipindi chote hicho watoto walikua wakimlilia Mama yao. Yaani wakilala wakiamka ni kuniuliza, wananiita anko, Mama yuko wapi (Mara nyingi wnaaniita anko), wanmauuliza Bibi yao Mama yuko wapi. Sasa kilichonifanya nilie nipale ambapo mtoto mkubwa wa miaka kumi ambaye anaelewa kitu kidogo alikua anampembeleza mdogo wake alikua anamuambia. “Us...

NILIKUPENDA ZAIDI WEWE.

Image
NILIKUPENDA ZAIDI WEWE. Hapo kale, alikuwapo msichana mrembo - kipofu. Kwa sababu ya upofu wake, alijichukia sana na kujikatia tamaa. Chembe pekee ya furaha aliyobakiwa nayo moyoni, ilitokana na upendo wa hali ya juu aliokuwa akitendewa na mpenzi wake. Alipendwa, alithaminiwa, alidekezwa na kuengwaengwa mithili ya mboni ya jicho. Ikafikia hatua, kwa mapenzi aliyopewa, msichana akaweka nadhiri kwamba, siku akibahatika kufumbua macho na kuiona dunia, basi ataolewa na mpenzi wake huyo bila mahari. Siku moja, alitokea mtu ambaye - inasemekana - alikuwa katika saa za mwisho wa uhai wake, akaamua kujitolea macho yake akampa msichana huyu, kwakuwa yeye hakuwa na maisha marefu tena. Na baada ya madaktari kumfanyia upasuaji msichana, na kumpandikizia macho yale, hatimaye msichana alifanikiwa kuona; aliona kila kitu pamoja na kumwona mpenzi wake. Mpenzi wake akamuuliza, "Hatimaye umeiona dunia. Je, uko tayari sasa kufunga ndoa nami?" Msichana alifadhaika mno baada ya kugundua kwamb...

HAINIHUSU MIMI TUSOME TUJIFUNZE ,TUSIKURUPUKE KUPATA UTAJIRI BILA JASHO.

Image
HAINIHUSU MIMI TUSOME TUJIFUNZE ,TUSIKURUPUKE KUPATA UTAJIRI BILA JASHO. Mimi ni mwanamke mjane ninaishi mjini Arusha. Huu ni ushuhuda wangu wa maisha yangu. Miaka 21 iliyopita nilifunga ndoa na mume wangu mpendwa kanisani, baadaye tukajaliwa kuwa na watoto wa2 mmoja wa kiume Alfred na mwingine wa kike Minza. Mimi nimesomea mambo ya uuguzi MD, nimefanya kazi muda mrefu ktk hospitali za wilayani karatu na Arusha mjini mpk nilipolazimika kuacha kutokana na udhaifu wa mwili na mambo yaliyonipata katika maisha. Mume wangu alikua ni askari polisi mpk baadaye alipojiunga na ajira zingine mpaka alipokutwa na mauti kama nitakavyoeleza baadaye hapo chini. Tulipooana na mume wangu,maisha yalikua ya furaha sana na tulikua na mipango mingi mizuri ya kujiendeleza kiuchumi na kihuduma kwani tulikua tunampenda Mungu na tulikua waimbaji na waombaji kanisani. Baada ya muda mrefu katika maisha ya ndoa na familia, baadaye maisha yalianza kuwa magumu kutokana na mishahara yetu kuwa midogo ukilinganisha...

Msanii Naseeb Abdul (Diamond) akamatwa na Polisi kwa kusambaza picha za faragha, Nandy naye ahojiwa

Image
Msanii Naseeb Abdul (Diamond) akamatwa na Polisi kwa kusambaza picha za faragha, Nandy naye ahojiwa Mwakyembe amesema kuna baadhi ya wasanii ambao walianza kufanya uhuni ndani ya mitandao akiwemo mwanamuziki nyota wa muziki, Diamond ambae tayari amekamatwa na Jeshi la Polisi na anahojiwa kutokana na picha alizozungusha. Pia Mwakyembe amesema pia imebidi binti Nandy naye akamatwe kisha kuhojiwa na wanaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani. Mwakyembe ametoa wito kwa vijana kuwa mitandao sio kokoro la kupeleka uchafu wote ambao umezuiwa na sheria zingine na nchi ina utamaduni wake ambapo inahitajika kulindwa kizazi cha sasa na cha kesho cha Taifa hili. Akiuliza swali, mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga alitaka kujua kauli ya serikali juu kukithiri kwa ushoga na kutukana matusi mithili ya bomu la nyuklia ambayo sio maadili ya mtanzania na team za matusi ikiwemo za Wema, Zari, Diamond na Shilole. Mwakyembe amesema sheria ya EPOCA ilitungwa mwaka 2010 lakini zilikosekana kanuni za kuban...

Mtoto mwenye umri wa miaka 16 alimuliza mama nikifikisha umri wa miaka 18 utanifanyia nin..?

Image
SOMA HII TAFADHALI Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 16 alimuuliza mama yake: "Mama, utanifanyia nini nikifikisha umri wa miaka 18 (siku yangu ya kuzaliwa) Mama akajibu:- "mwanangu bado una unasafari ndefu". mtoto yule lifikisha umri wa miaka 17, siku moja ghafla akaanguka chini. Mama yake akambeba na kumuaisha hospitali, na daktari akasema: "Mama mwanao ana Moyo mkubwa pia limeonekana tundu katika moyo wake." Mama akiwa na mwanae pale hospitali huku mama akiwa na mawazo nini cha kufanya, mtoto akamuuliza mama yake " Mama Madaktari wamekwambia mimi ninaenda kufa?? Mama akaanza kulia.. Baada ya muda wa mwaka nzima kijana huyu akiwa amefikisha mika 18 alirudishwa nyumbani kutokana na hali yake kuwa nzuri. baada ya kufika nyumbali alikuta barua ipo kwenye kitanda, iliyokuwa imeandikwa na mama yake. Barua iliandikwa hivi: Mwanangu unasoma haya kwa sababu kila kitu kimeenda sawa mpaka sasa. kumbuka siku uliyoniambia siku ukifikisha miaka 18 nitakupa nini n...

HABARIACT Wazalendo wabaini maeneo nane hatari katika ripoti ya CAG, Watoa mapendekezo yao

Image
HABARIACT Wazalendo wabaini maeneo nane hatari katika ripoti ya CAG, Watoa mapendekezo yao Leo Jumapili Aprili 15, 2018 Chama cha ACT Wazalendo kimetoa tathmini na uchambuzi wake juu ya ripoti  mpya ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2016/17. Zitto Kabwe Soma taarifa hiyo iliyotolewa leo Aprili 15, 2018 na Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG, Prof. Mussa Assad ametoa taarifa yake ya ukaguzi wa mapato na matumizi ya fedha za umma kwa mwaka 2016/17. Kwa sasa taarifa hiyo iko wazi kwa umma, baada ya kuwa imekabidhiwa rasmi bungeni. Sisi ACT Wazalendo, tumeisoma, kuipitia na kuichambua taarifa husika, kwa lengo la kuitumia ili itusaidie kutimiza wajibu wetu wa kuisimamia Serikali, kama chama cha Upinzani bungeni. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu Magufuli tayari amechukua hatua za kiuwajibikaji dhidi ya baadhi ya Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa zenye ha...

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  KUDUMAA, KUSINYAA, KUNYWEA NA  KURUDI  NDANI  KWA  MAUMBILE  YA  KIUME PAMOJA  NA  TIBA  DHIDI  YA MAUMBILE  YA  KIUME  YALIYO  DUMAA NA KUSINYAA  KWA  SABABU  YA  PUNYETO.

Image
JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  KUDUMAA, KUSINYAA, KUNYWEA NA  KURUDI  NDANI  KWA  MAUMBILE  YA  KIUME PAMOJA  NA  TIBA  DHIDI  YA MAUMBILE  YA  KIUME  YALIYO  DUMAA NA KUSINYAA  KWA  SABABU  YA  PUNYETO. Kudumaa , kusinyaa  na  kunywea  au kurudi ndani  kwa  uume  ni tatizo  linalo  wakabili wanaume  wengi  duniani. Dalili  za  tatizo  hili  ni  pamoja  na  kuwa na  maumbile madogo sana yaliyo dumaa, sinyaa  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuyafanya  yaonekane  kama  ya  mtoto  mdogo. VYANZO  VYA  TATIZO  LA  KUDUMAA  NA  KUSINYAA  KWA  MAUMBILE  YA  KIUME. Kwa  mujibu wa  tafiti  mbalimbali  za  kisayansi, tatizo la  kudumaa  na...

MAKALAMakala: Nandy umetudanganya, umezidi kumpa ushindi Zari 

Image
Kwanza nitoe pole kwa Nandy na Bill Nass mara baada ya video yao ya faragha kuvuja mtandaoni, ni kitu ambacho unaweza kukichukulia kawaida ila uisiombe yakukute. Viatu walivyovaa Nandy na Bill Nass kwa sasa vinawapwaya katika miguu yao na pengine ni vizito, nitoe pole kwao kwa hilo lilowafika kwani ni tukio ambalo si vigumu kuja kufutika katika maisha yao kutokana na utandawazi uliopo sasa. Fid Q katika ngoma yake August 13 alisema, ustaa ni mzigo wa mwiba, ukiubeba utaumia. Video ya Nandy na Bill Nass imesambaa kwa kasi kutokana na umaarufu wao, hivyo maumivu wanayopitia wanapaswa kuelewa ni kawaida katika tasnia yao ya burudani. Nandy ameelewa hilo na ndio sababu hakuona aibu kuomba radhi kwa mashabiki wake kwa hicho kilichotokea. Kwa anayeelewa maana ya neno samahani atakuwa amemsamehe na maisha mengine kuendelea. Kwanini Nandy Baada ya video kusambaa, Nandy na Bill Nass kila mmoja amejitetea kwa upande wake. Nimzungumzie Nandy kwa ufupi; ameomba radhi na kueleza kilichotokea i...

TAFAKARI LEO

Image
TAFAKARI YA LEO Kijana huyu wa mtaani huwa kila mara anaomba pesa kwenye magari, alivyosogelea gari la huyu mama pichani alimuona ana mtungi mkubwa wa gesi, (ukiangalia picha kwa karibu utauona). Akamuuliza "mama huo mtungi ni wa nini"? Mama akamjibu ni wa kuupa (supply) mwili wangu na hewa ya Oxygen. Huyu kijana pichani akalia sana kama anavyoonekana. Huyu mama anaishi kwa kutembea na mtungi wa gesi pamoja na ka jenereta kadogo popote anakoenda ili mwili uweze (kupumua) kupata hewa ya oxygen. Na hii ndio hali ya huyu mama kwa miaka mingi iliopita. Huyu mtoto alijiona mwenye afadhali na asie na shida na akaomba msamaha kwa Mungu kwa kulalamikia hali alioko nayo ya maisha duni. CHA KUJIFUNZA HAPA Usimlaumu Mungu kwa hali ulioko nayo kwasasa omba Mungu rehema zake ziwe juu yako na hakika kuna siku Mungu atakuinukia pale ulipo. Mungu sio mkatili mpaka akuache uteseke kiasi hicho. Kama unahuitaji leo hii sukuma maombi yako na sadaka, inenee sadaka yake mwambie Mungu shida y...

Mbwa mwenye umakini ktk majambo

Mbwa mwenye umakini

Mtoto mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Fred Lowassa, ameshangaa mwanamke aliyejitokeza na kudai kuwa ni binti wa mwanasiasa huyo.

Image
Mtoto mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Fred Lowassa, ameshangaa mwanamke aliyejitokeza na kudai kuwa ni binti wa mwanasiasa huyo. Aidha, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutumia vizuri mamlaka yake. Kauli hiyo ya Fred imekuja saa chache baada ya mwanamke mmoja mkazi wa Kigamboni, Fatuma Lowassa (31), kujitokeza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, leo Jumanne Aprili 10, akidai kutelekezwa na baba yake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa. Akiwa Monduli mkoani Arusha, Fred ametoa tamko akisema; “Nimesikia mwanamama mmoja akiongea kuwa yeye ni ndugu yetu kule Dar es Salaam. “Kwa taarifa tu sisi watu wa Monduli kwetu watoto ni baraka na neema, nimeshangaa ametukosa ukoo mzima kujitambulisha. “Namwambia Paul Makonda, nimetoka naye mbali sana, nasikitika sana anavyotumia nafasi yake vibaya kwa manufaa anayoyajua. Makonda nimekulea.” Ameandika Fred. Mwanam...

Mke wa nane wa Mfalme wa Swaziland, Mswati (III), Senteni Masango amefariki dunia akiwa chumbani kwake wikiendi iliyopita.

Image
Mke wa nane wa Mfalme wa Swaziland, Mswati (III), Senteni Masango amefariki dunia akiwa chumbani kwake wikiendi iliyopita. Senteni Masango Vyombo vya habari nchini Swaziland vimeeleza kuwa Bi. Masango alitumia dawa aina ya AMITRIPTYLINE kupita kiasi (Overdose) kitu ambacho kimepelekea mwanamke huyo kupoteza masiha, hii ni baada ya mwili wake kufanyiwa uchunguzi na madaktari nchini humo. Kwa mujibu wa mtandao wa Face 2 Face umeeleza kuwa Bi. Masango alichukua uamuzi huo wa kujiua Ijumaa ya Aprili 07 ya wiki iliyopita, Baada ya mumewe kumkataza kuhudhuria kwenye mazishi ya dada yake yaliyofanyika Jumapili ya Aprili 01, 2018. Kufuatia tukio hilo, tayari serikali nchini Swaziland kupitia kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Dkt. Sibusiso Dlamini imetuma salamu za rambi rambi kwa familia ya Mfalme Mswati (III). Bi. Masango aliolewa na Mswati (III) mwaka 1999 na ameacha watoto wawili wa kike na leo Aprili 10, 2018 mwili wake unatarajiwa kuzikwa kwa heshima nchini humo.

HABARISerikali yavunja rekodi ukusanyaji mapato kwa mwaka mpya wa fedha wa  2017-2018.

Image
HABARISerikali yavunja rekodi ukusanyaji mapato kwa mwaka mpya wa fedha wa  2017-2018. Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA) imevunja rekodi katika ukusanyaji wa mapato kwa miezi tisa ya mwaka mpya wa fedha wa 2017/18 kuanzia Julai, 2017 hadi Machi, 2018 . Richard Kayombo Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Aprili 10, 2018 na Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi (TRA), Richard Kayombo imeonesha kuwa serikali kwa miezi tisa imekusanya kiasi cha tsh Trilioni 11.78 likiwa ni ongezeko la ukuaji kwa asilimia 8.46%, ukilinganisha na mapato yaliyokusanywa kwa mwaka wa fedha uliopita wa 2016/17 ambapo serikali ilikusanya kiasi cha Tsh Trilioni 10.86 . Bwana Kayombo amesema kuwa mafanikio hayo ya ongezeko la kodi yametokana na elimu iliyotolewa kwa Wananchi juu ya ulipaji kodi na uzalendo kwa watendaji kazi wake kumechangia kufikia makusanyo hayo.

KIJANA WETU ANAPITA KWENYE MATESO YA DUNIANI

Image
KIJANA WETU ANAPITA KWENYE MATESO YA DUNIANI (Wakati sisi tunayapita,yeye anayapitia matatizo) Mtoto MUDASILI amezaliwa Septemba 2016 katika kijiji cha Nampemba wilayani Nachingwea mkoani Lindi anasumbuliwa na tatizo la uvimbe katika jicho la kushoto. Mama mzazi wa mtoto bi Hadija Saidi alizungumza nami juu ya ujio wa tatizo la kijana wake. "Mwaka jana mtoto alianza kujiwasha jicho hili,hali ambayo ilinilazimu kwenda hospital huku jicho la mtoto likiwa jekundu mithiri ya damu'' Tulipewa dawa tukarejea nyumbani,hata hivyo hazikusaidia. Kadiri siku zilivyosonga hali jicho la mtoto ilizidi kuwa mbaya,hali iliyopelekea jicho kutokea kwa nje kama unavyoona tukaenda Ndanda nako tukaambiwa tuende Nyangao. Siku chache baadae tulipewa rufaa ya kwenda Muhimbili huko ambako tuliambiwa mtoto ana SARATANI ambayo imeenea mwiilini,hivyo turejee nyumbani hakuna tiba mbadala zaidi ya kupata dawa za kupunguza maumivu tu. Hali ilivyozidi kuwa mbaya baba wa mtoto alimkana kutokumtambu...

JOYCE KIRIA AJITOKEZA KWA MAKONDA, WALIOTELEKEZWA WAMINIMIKA! – PICHAZ

Image
JOYCE KIRIA AJITOKEZA KWA MAKONDA, WALIOTELEKEZWA WAMINIMIKA! – PICHAZ Mwanaharakati wa masuala ya usawa wa kijinsia na Mtangazaji wa kipindi cha ‘Wanawake Live’, Joyce Kiria ‘Super Woman’ (mwenye hereni pichani) amekuwa mmoja ya mamia ya wanawake waliojitokeza leo, Aprili 09, 2018 kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupatiwa msaada wa kisheria baada ya kutelekezewa watoto na wazazi wenzao. Mamia ya wanawake wamemiminika leo katika ofisi hizo kufuatia wito wake kuwataka wanawake wote waliotelekezewa watoto na wazazi wenzao wa kiume wafike ofisini hapo na vielelezo halali ili waweze kupatiwa msaada wa kisheria. Wanawake hao ambao kwa sasa wanalea watoto wao peke yao baada ya kutelekezwa, wamejitokeza kuanzia majira ya asubuhi japo kuwa mvua kubwa zilikuwa zikinyesha. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kiria ameandika; Dar Es Salam Mpya! Wanawake tuliotelekezwa tunalea familia peke yetu! Makonda ameanza rasmi kusikiliza shida za w...
Image
salim msangi TAIFA TEULE na URONGO WA ZAMA ZOTE Pt 3 Watu wa kwanza wa Khazairi walijulikana kama Ashkenazi na Sephardic. Wa Khazairi wa Ashkenazi ambao ni sehemu ya watu wanaojiita Wayahudi leo na ambo ndani ya Israeli ni wengi kulinganisha na wenzao na ndiyo wao wanaoshikilia madaraka tangu nchi ya Israeli ilipoanzishwa mwaka 1948 hawahusiani chochote na Wayahudi waliotajwa katika Biblia.  Katika Biblia Ashkenaz wametajwa kama watu waliokuwa wakiishi katika milima ya Ararat (Uturuki ya leo) na Armenia maeneo ambayo kama tulivyo ona mwanzo kuwa ndiyo yalikuwa makazi ya Khazairi. Baada ya kuporomoka kwa dola yao watu hawa hawakuwa wakizungumza lugha ya Kisemitik ya Kiyahudi, na hiyo si ajabu kwani wao si Wayahudi bali walikuwa na lugha yao wenyewe yenye machanganyiko na maneno ya lugha tofauti hasa ya jamii ambazo wameingiliana nazo ikiwemo jamii ya Wayahudi na lugha hiyo waliita  Yiddishi. Lugha hii haikutokea Palestina bali Ulaya ya Kati ikiwa na lahaja za Kij...