Siasa na Mabepari.

Mtoto mdogo alimfuata baba yake na
kumuliza, "Nini maana ya SIASA?". Baba
akajibu, "Mwanangu, ngoja nijaribu kujibu
kwa mfano huu. Mimi natafuta fedha ya
matumizi, hivyo niite mimi BEPARI, Mama
yako yeye anasimamia matumizi ya fedha,
hivyo mwite SERIKALI.
Mimi na mama yako tuko kwa ajili ya
kuwapa nyie mahitaji yenu, hivyo nyinyi
twawaita WANANCHI. Dada wa kazi yeye
anatusaidia kazi za hapa ndani hivyo
tunamwita MFANYAKAZI. Na mdogo wako
ambaye ni mdogo tumwite FURSA ZA
BAADAYE.
Haya sasa mwanangu hebu fikiri na uone
kama ninakupa jibu la kuridhisha! Kijana
akaondoka na kwenda kulala huku akifikiri
na kuyatafakari maneno aliyoyasema
baba. Baadae usiku ule, akasikia mtoto
ambaye ni mdogo wake akiwa analia hivyo
akaamua kuamka na kwenda kumcheki.
Akaona mtoto kajinyea na kajipaka uchafu
huo huku akilia kuashiria anahitaji msaada.
Akaamua aende chumbani kwa baba na
mama, akamshuhudia mama akiwa peke
yake kalala usingizi mzito na hana habari
yoyote. Hakutaka kumwamsha akaona
angemsumbua mama, akarudi na kwenda
chumba cha dada wa kazi na kuona
mlango umefungwa.
Akachungulia kupitia tundu la ufunguo na
kuona dada wa kazi akiwa na baba.
Akakata tamaa na kurudi kulala bila ya
kuwa na msaada wowote kwa mdogo
wake.
Siku ya pili mtoto akamwambia baba,
"Sasa nafikiri naelewa maana halisi ya
SIASA." Baba akasema, "Safi sana mtoto
mzuri, haya sasa niambie kwa maneno
yako maana halisi ya siasa kwa jinsi
ulivyoitafakari".
Mtoto akajibu, "Ni hivi, wakati BEPARI
anamyanyasa na kumtumia vibaya
MFANYAKAZI, SERIKALI imelala usingizi
mzito, Na WANANCHI hawasikilizwi shida
zao huku FURSA ZA BAADAYE zikiwa
zimesusiwa kwenye uchafu bila msaada.
Baba kidogo azimie
🤣🤣🤣🤣🤣

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!