FAHAM TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
FAHAM TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Nguvu za kiume: Huu ni uwezo wa mwanaume katika kustahimili kufanya tendo la ndoa.
FAIDA ZA TENDO LA NDOA.
i) Huongeza kinga za mwili; huongeza nguvu ya kinga ya mwili(Immunoglobin A) hivyo husaidia kutougua magonjwa mbali mbali.
ii) Huimarisha afya ya moyo; hupunguza ugonjwa wa moyo kwa 45% kwa wanaofanya walau Mara 6 kwa mwezi kuliko wanaofanya Mara moja kwa mwezi na pia hupata faida ya mazoezi na kuleta uwiano sawa wa testosterone na estrogen ambazo ni muhim kwa afya ya homoni ya mwanaume na ya moyo na mishipa ya dam(Cardiovascular system)
iii) Hupunguza msongo wa mawazo, shinikizo la damu(Presha ya kupanda au kushuka), na kuboresha misuli ya mgongo,kiuno,kifua hivyo ni zoezi tosha.
iv) Hupunguza maumivu; Hisia nzuri za tendo la ndoa huzalisha homoni zinazosaidia kupunguza maumivu ya miguu, mgongo, sehem za maungio na kichwa.
V) Huzuia Saratani ya Tezi Dume, kwa kumwaga shahawa Mara 21 kwa mwezi yaani Mara 5 kwa week nikimaanisha kufanya tendo la ndoa Mara 2 kwa week husaidia kuondoa mashambulizi ya saratani hiyo.
Vi) Huboresha Usingizi; Baada ya tendo homoni inayohusika na kupooza mwili(Prolactin) hutolewa na kuruhusu kupata usingizi wa mapema na pia homoni ya mapenzi(Oxytocin) hutolewa wakati wa kufika kileleni na kufanya upate usingizi mapema.
Vii) Huimarisha Uhusiano; pale ambapo kila mmoja wapo anakidhi haja ya mwenza wake kwa wakati sahihi hufanya wote wakijisikia wapya kila wafanyapo tendo na kuzidi kuimarisha uhusiano wao.
TATIZO LA NGUVU ZA KIUME
Hii hutofautiana kwa mwanaume mmoja na mwingine kwasababu katika maisha ya kila siku wanaume tumekuwa tukipambana sana kwa kutumia akili na nguvu zetu zote kuhakikisha tunatimiza mahitaji katika familia zetu kama ilivyoandikwa katika maandiko kuwa tutakula kwa jasho letu na si vinginevyo, hii hupelekea wanaume wengi kukosa uwezo wa kuwaridhisha wenza wao katika tendo muhimu kwa afya na akili kiujumla Na kusababisha kutokea kwa dalili zifuatazo;
a) Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume barabara.
b) Kukosa ham ya tendo la ndoa.
c) Kutokuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya Mara moja.
d) Kufika kileleni mapema.
e) Kutokuwa na uwezo wa kisimamisha uume kabisa.
f) Uume kusinyaa na kurudi ndani.
SABABU ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.
i) UMRI; kuanzia miaka 61 hupata tatizo hili zaidi kuliko miaka 41 kushuka chini kutokana na baadhi ya tishu katika mzunguko wa dam
kuzalishwa chache zaidi hivyo kupunguza ham ya tendo.
ii)Kutofanya mazoezi ya viungo mara kwa mara; Hii hufanya mzunguko wa dam kuwa mdogo pasipo kawaida na kusababisha hata hisia au mihemko kuwa chini pia maana dam itashindwa kupita vizur kwa usahihi na kusababisha uume usisimame barabara.
iii) Unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara kupita kiasi; hii husababisha mwili kuondosha virutubisho muhimu kwenye homoni ya mwanaume kama Madini ya Zinc, Vitamini B6 na Selenium ambavyo huwa kama ni vichochezi na kumsaidia vizur sana mwanaume wakati wa tendo.
iv) Msongo wa mawazo(Stress);
Haya ni mabadiliko ya kisaikolojia katika mfumo wa faham kutokana na stail ya maisha tunayoishi kama Madeni,hasara katika biashara, kutojaliana, uwoga ambavyo huondoa ham ya kufanya tendo.
v)Magonjwa yasiyo ambukizi; kama presha(kupanda au kushuka), kisukari, kiharusi, saratani ya tezi dume na matatizo ya moyo ambayo husababishwa na mifumo mibovu ya ulaji wa vyakula katika kuweka uwiano sawa wa vyakula vya wanga, protini, vitamin na mafuta.
vi) Matumizi holela ya dawa bila kushauriwa na wataalamu wa afya; haya mazoea ni mabaya sana maana utumiaji wa dawa hizi hutoa kemikali ambazo huweza kuharibu mfumo wa UZAZI na kuathiri mfumo wa dam kupitia mishipa na kupunguza hisia au ham ya tendo.
vii) Kuendesha Vyombo ya usafiri kwa umbali mrefu na Mara kwa Mara; hii pia inamadhara sababu huzifanya korodani ambazo ndo hutunza homoni za mwanaume(Testosterone) zitumikazo kuzalisha mbegu za kiume kubwana mara kwa Mara sababu ya kukaa kwenye kiti mda mrefu na kusababisha upungufu wa uzalishaji wa mbegu na mzunguko wa dam kiujumla.
viii) Kujichua au Kupiga punyeto;
Kitendo hiki ni moja ya sababu kubwa sana tena sana maana husababisha ule mshipa unaotoa damu(Vena) kulegea wakati ulitakiwa ubanwe ili kuipa nafasi mishipa inayoingiza dam(Ateri) iingize kwa wingi kwenye mishipa ya uume, hivyo kupelekea kuwahi kufika kilekeni mapema maana dam itakuw imeshaondoshwa kwenye mishipa ya uume na kuufanya usisimame barabara kwa mda mrefu na kusababisha kusinyaa na kukosa nguvu hivyo kukosa ham au kushindwa kurudia tendo tena na tena.
KWA USHAURI ZAIDI JUU YA UFUMBUZI WA TATIZO HILI NAPATIKANA KWA NAMBA ZIFUATAZO;
0769 280 233.
0715 280 233.
Whatsapp number +255715 280 233
Comments
Post a Comment