HABARISerikali yavunja rekodi ukusanyaji mapato kwa mwaka mpya wa fedha wa  2017-2018.

HABARISerikali yavunja rekodi ukusanyaji mapato kwa mwaka mpya wa fedha wa  2017-2018.

Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA) imevunja rekodi katika ukusanyaji wa mapato kwa miezi tisa ya mwaka mpya wa fedha wa 2017/18 kuanzia Julai, 2017 hadi Machi, 2018 .

Richard Kayombo

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Aprili 10, 2018 na Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi (TRA), Richard Kayombo imeonesha kuwa serikali kwa miezi tisa imekusanya kiasi cha tsh Trilioni 11.78 likiwa ni ongezeko la ukuaji kwa asilimia 8.46%, ukilinganisha na mapato yaliyokusanywa kwa mwaka wa fedha uliopita wa 2016/17 ambapo serikali ilikusanya kiasi cha Tsh Trilioni 10.86 .

Bwana Kayombo amesema kuwa mafanikio hayo ya ongezeko la kodi yametokana na elimu iliyotolewa kwa Wananchi juu ya ulipaji kodi na uzalendo kwa watendaji kazi wake kumechangia kufikia makusanyo hayo.

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!