KIJANA WETU ANAPITA KWENYE MATESO YA DUNIANI

KIJANA WETU ANAPITA KWENYE MATESO YA DUNIANI
(Wakati sisi tunayapita,yeye anayapitia matatizo)

Mtoto MUDASILI amezaliwa Septemba 2016 katika kijiji cha Nampemba wilayani Nachingwea mkoani Lindi anasumbuliwa na tatizo la uvimbe katika jicho la kushoto.

Mama mzazi wa mtoto bi Hadija Saidi alizungumza nami juu ya ujio wa tatizo la kijana wake.
"Mwaka jana mtoto alianza kujiwasha jicho hili,hali ambayo ilinilazimu kwenda hospital huku jicho la mtoto likiwa jekundu mithiri ya damu''
Tulipewa dawa tukarejea nyumbani,hata hivyo hazikusaidia.

Kadiri siku zilivyosonga hali jicho la mtoto ilizidi kuwa mbaya,hali iliyopelekea jicho kutokea kwa nje kama unavyoona tukaenda Ndanda nako tukaambiwa tuende Nyangao.

Siku chache baadae tulipewa rufaa ya kwenda Muhimbili huko ambako tuliambiwa mtoto ana SARATANI ambayo imeenea mwiilini,hivyo turejee nyumbani hakuna tiba mbadala zaidi ya kupata dawa za kupunguza maumivu tu.

Hali ilivyozidi kuwa mbaya baba wa mtoto alimkana kutokumtambua mtoto wako na kuondoa mahusiano.

Ndugu zangu!
Mtoto wetu anapita kwenye wakati mgumu
Anahitaji msaada wa kiroho  na pesa za chakula,huu ni mwaka wa pili mamae hana nafasi hata ya kushika jembe kwa kukosa muda wa kufanya shughuli za uzalishaji hali inayopelekea familia kukosa mahitaji muhimu.

Hali ya uvimbe imeingia hadi ndani ya koo,hali hii inamsababishia Mudasili kutoweza kula chakula kigumu na kuhitaji hakula laini na kunywa madawa ya kukata maumivu "PAIN KILLER" na dawa za kupambana na wadudu kwenye jeraha.

HUDUMA
Baada ya kuliona tatizo hili kwa hatua hii
Familia yangu imejitolea kumlipia bili ya maziwa kwa mwezi mmoja
Nimekwenda kumfariji mama wa mtoto kwa kumpa elimu ya kiroho pia kumuunganisha na jumba la ibada(Msikiti) kwa kufanya kikao na wazee wa msikiti kuwajuza namna gani bi Hadija anapaswa kutunzwa kwa kipindi hiki cha mpito.

Ndugu zangu
Kwa kupitia ombi langu juu kuwaombeni msaada hili niweze kufanya safari ya kumfikia mtoto anaelia huku watu hawamsikii,anaeita watu hawaitiki wala kuguswa mateso yake nimepata pesa 153,000/=
Pesa hizi nakwenda kumsaidia MUDASILI zimsaidie kwa chakula na usafiri wa kuhudhuria hospitali pale anapohitajika kufanya hivyo.

RAI YANGU
Kwa watakaoguswa kumsaidia mtoto na mama yake
Hii ni namba ya Bi HADIJA SAIDI 0654197916
(Namba hii imesajiliwa kwa jina la kiume ni vema ukipiga ujiridhishe)
Wale watakaoguswa kupitia kwangu unaweza kuniomba/kunipa muongozo na msaaa utafika.

Poleni kwa picha za hudhuni
Shukrani kwa michango yenu hamjaitupa imeenda aalikoilekeza Mungu.
Mungu awajalie kuwajazia mlipotoa.

"KWA UPENDO WETU MTOTO ATAONGEZA SIKU ZA KUISHI KWAKE TUMSAIDIE KWA DUA NA SALA"

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!