Posts

Showing posts from March, 2018

SOKO LA MADINI LAANZISHWA MWANZA

Image
SOKO LA MADINI LAANZISHWA MWANZA: Serikali imeridhia kuanzishwa kwa soko la madini mkoani Mwanza ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na utoroshwaji wa madini nje ya nchi. Soko hilo linalotarajiwa kuanzishwa kwenye jengo la kibiashara la Rocky City mall lililopo manispaa ya Ilemela jijini humo. “Kamati ilifanya utafiti katika maeneo mbalimbali ya jiji hili na ikagundua kwamba Rock City mall inavigezo vya kuwa soko la madini kwa asilimia kubwa,” alisema mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo John Bina. Soko hilo linatarajiwa kuwa la kudumu na litafanya kazi kila siku  ikiwa ni mapendekezo ya kamati iliyoundwa na Naibu waziri wa madini Stanslaus Nyongo  ili kufanya uchunguzi wa kina kuhusu utoroshwaji wa madini. Kamati pia ilitoa pendekezo la kufungwa kwa mitambo ya kisasa katika uwanja wa ndege wa Mwanza kufuatia kuwepo kwa mitambo ambayo inashindwa kugundua dhahabu inayotorishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu.

TEMBO ANAYETOKA MAJIVU YA MOTO MDOMONI:

Image
TEMBO ANAYETOKA MAJIVU YA MOTO MDOMONI: Wanasayansi pamoja na wataalamu wa wanyama pori duniani, wamepigwa bumbuwazi baada ya kuonekana kwa tembo anayetoa majivu yanayogeuka kuwa moto huko India. Wanasayansi wanasema mpaka sasa hawaelewi ni kwa nini tembo huyo alikuwa anatoa majivu. Vinay Kumar ni mwanasayansi wa hifadhi ya wanyama pori katika jamii ya watu wa India,alipiga picha ya video ya sekunde 48 wakati yuko katika safari ya kikazi katika msitu wa Nagarhole katika mji wa Karnataka mwezi april mwaka 2016. Aliwaambia BBC kwamba hakuionyesha video hiyo mapema  kwa sababu hakutambua umuhimu wake. Bwana Kumar amesema yeye na wenzie walitembelea katika msitu huo nyakati za asubuhi ili kuona kama camera zao walizoziweka zimewapiga picha chui. Lakini wanakuta imempiga picha tembo wa kike aliyekuwa katika umbali wa mita 50 wa kamera.

MAKOSA 13 KATIKA PESA AMBAYO HUTAKIWI KUYAFANYA

Image
MAKOSA 13 KATIKA PESA AMBAYO HUTAKIWI KUYAFANYA   1 Usikope pesa ya riba ili uanzishe biashara. Usitegemee pesa ya mkopo kuianzishia biashara, upate faida kisha uirudishe pesa ya mkopo na riba yake.    2 Usitumie pesa ambayo bado haipo mikononi mwako. Wala usije ukamuahidi mtu kumpa pesa ambayo  umeahidiwa mahali fulani. Kama kuna mtu kakwambia, Flan njoo kesho nikulipe deni lako" Basi wewe usiende kukopa vitu kadhaa dukani au hata kumuahidi mtu mwingine kumpa pesa ambayo na wewe umeahidiwa.  Ni kosa. Unaweza kuingia kwenye matatizo.    3 Kama unataka kuhifadhi/kutunza pesa, kila unapopata pesa usianze kuitumia kwanza kisha ukategemea kutunza kiasi kitakachosalia. Hivyo basi,  ukipata tu pesa,  weka pembeni kiasi unachodhani kinafaa kutunzwa/kuhifadhiwa kisha tumia kiasi kilichobaki.       4 Ukipata nafasi ya kuonana na mtu tajiri, kamwe usiombe pesa.  Omba maarifa ya kutengeneza pesa kama yeye, tena kwa ...

SERIKALI IMESEMA ITAGHARAMIA MAZISHI YA KIJANA ALEN ACHILES ALIYEFARIKI MKOANI MBEYA.

Image
SERIKALI IMESEMA ITAGHARAMIA MAZISHI YA KIJANA ALEN ACHILES ALIYEFARIKI MKOANI MBEYA...soma zaidi👇👇👇👇👇👇 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo,William Ntinika amefunguka na kuweka wazi kuwa serikali itagharamia mazishi ya kijana Alen Achiles (20),aliyefariki muda mfupi baada ya kutoka polisi.👇👇👇👇👇 ------------------------------- Mkuu wa wilaya huyo ambaye alifika nyumbani kwa wazazi wa marehemu na kutoa rambirambi ya laki mbili na kuahidi kuwa serikali itagharamia mazishi ya kijana huyo ikiwa pamoja na kukodi gari la matangazo pamoja na chakula.👇👇👇👇👇 Hata hivyo jeshi la polisi mkoani Mbeya limekana kuhusika na kifo cha kijana huyo na kusema kuwa kijana huyo alitoka mikononi mwa Jeshi hilo na kuondoka na ndugu zake baada ya kudhaminiwa ak...

Yote yaliyogonga katika Magazeti ya leo March 25,2018

Image
Karibu tumekuletea yote yaliyojili katika Magazeti ya Leo March,25,2018

ONYO! USITUMIE MBEGU ZA KISASA

Image
salim msangi ONYO! USITUMIE MBEGU ZA KISASA Watu wachache kabisa na wamiliki wa kampuni chache tu, lakini kampuni kubwa mno duniani, watu hao nyuma ya kampuni hizi wanafanya kila wawezalo usiku na mchana kumiliki kila punje ya mbegu iliyopo kwenye uso wa dunia. Msukumo wa mbegu za kisasa dhidi ya zile za asili ni mkubwa mno katika dunia ya leo kupitia matangazo ya biashara na taasisi za kiserikali. Kiasi kwamba inaonekana tegemeo la dunia ijayo kwenye chakula lipo kwenye mbegu za kisasa pekee. Hitajio la viwanda na uroho, ulafi wa watu wachache kutaka kumiliki uzalishaji wa mbegu zote duniani kupitia makampuni yao ya kimasonia. Ili kamapuni hizo kujihakikishia umiliki wa mbegu zote duniani ndipo walipo kuja na wazo la GMO (GENETIC MODIFIED seeds, crops, animals etc) Mbegu hizi za kisasa zinawazuia wakulima kuotesha mbegu zao wenyewe, kila msimu wa kilimo lazima ukanunue mbegu mpya. Moja ya matatizo makubwa kwenye uso wa dunia ya leo ni njaa, ambayo imeenea katika kila ...

MALIGHAFI ZA AFRIKA NA DAMU YA WAAFRIKA

Image
salim msangi MALIGHAFI ZA AFRIKA NA DAMU YA WAAFRIKA Tangu yalipo anza machafuko Rwanda 1990, Washington walikuwa na ajenda ya siri ya kusimamisha NGOME YA MAREKANI ndani ya Afrika ya kati, eneo ambalo kihistoria lilimilikuwa na Ufaransa na Ubelgiji. Mpango wa Marekani ulikuwa ni kumuondoa Ufaransa ndani ya Afrika ya kati (WASOMI NA WALE WENYE AKILI TUJIULIZE IKIWA RWANDA ILIKUWA NCHI HURU, KWANINI MAREKANI IPIGANE KUMUONDOA MFARANSA?) Mpango huo ulilenga kuwatumia Rwanda Patriotic Front (RPF), Washington ikawadhamini RPF kwa silaha, mafunzo na mbinu za kijeshi na vifaa. Kutokea katikati ya miaka ya kwenye miaka 1980, serikali ya Kampala chini ya Yoweri Musaveni, ilitumia na Washington kama mfano wa kuigwa kwa ‘demokrasi.’ Lakini pia Uganda ikawa ndiyo kituo ambacho waasi waliokuwa wakidhaminiwa na Washington, waliondokea hapo kwenda kufanya uasi wao kwenye nchi za Sudan, Rwanda na Congo. WANAWAFUNDISHA WAAFRIKA NAMNA YA KUUWANA Meja Jenerali Paul Kagame, alikuwa ...

PICHA ZA UCHI KWENYE MTANDAO NI BOMU NDANI YA NDOA

Image
salim msangi PICHA ZA UCHI KWENYE MTANDAO NI BOMU NDANI YA NDOA Ili uweze kuielewa posti hii vyema ni lazima uwe imeshaisoma posti iliyotangulia yenye maudhi kama haya inayo kwenda kwa jina  wa nikitazama picha za uchi kwa kiasi kikubwa sana tangu nikiwa ‘teeneger’ na nimekuwa na tatizo la ED tangu miaka ya ishirini, lakini ni kwenye miaka ya thelathini ndiyo tatizo la ED limekuwa jinamizi. Nimekuwa nikiwalaumu wanawake au mwenza kwa kukosa mvuto, au nikisingizia hili na lile kuhusiana na afya yangu, chakula, uchovu, umri n.k.  Lakini iliofikia wakati kwamba hata siwezi kupata nyege mshindo kwenye punyeto bila kutizama mtandao wa picha za uchi, kitu kikanigonga kwenye akili yangu..." Imekuwa ni kawaida kwa mtumiaji mkubwa wa picha za uchi kushinda kuhusisha tatizo la ED na filamu hizo. Hii hapa ni hadithi nyingine ya mwaathirika wa picha za uchi. “Nina miaka 24 na kwa miaka kadhaa nimekuwa nikipambana na tatizo la ED, na hivi karibuni tu ndiyo nimeweza kuona uh...

IKO WAPI NDEGE YA MALYSIA MH 370?

Image
IKO WAPI NDEGE YA MALYSIA MH 370? Mimi binafsi nililitilia shaka suala zima la ndege ya Malaysia kutoweka angani na isipatikane kokote kwenye uso wa dunia mpaka hivi leo, bado nalitia mashaka suala hilo kwamba halina ukweli wowote ndani yake, bali ni moja kati ya filamu zao nyingi wanazo ziigiza ilikuendelea kuulaghai umma, lakini zaidi mimi naona ni hayo niMAANDALIZI YA KUMTAFUTA ADUI MPYA ATAKAYE CHUKUA NAFASI YA ‘VITA DHIDI YA UGAIDI’. Kaa vizuri hapo ulipo ... Kwa kuanzia tu, tuitazame moja ya nambari kuu zinazo pendelewa kutumiwa kishetani na Illuminanti, nambari 11, zaidi kuhusu nambari hii tazama posti hii  Wakati ndege hiyo ya Malaysia ikipotea ndani yake kuliwa na abiria 227, nambari hiyo ni sawa na 2+2+7=11, ndege yenyewe ni Boeing 777 nambari inayogawika kwa 11. Ndege hiyo ya Malaysia ilipatwa na ‘ugonjwa’ kama ule uliozipata ndege za 9/11 ambayo tunajua kuwa tukio lile lilifanywa na utawala wa Bush mwenyewe. 1.          Ndege...

WAZIRI MWAKYEMBE AKERWA NA KAULI ZA DIAMOND

Image
WAZIRI MWAKYEMBE AKERWA NA KAULI ZA DIAMOND Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kukerwa na mwanamuziki Diamond Platnumz kutokana na kumdharirisha naibu wake Juliana Shonza wakati akihojiwa katika kipindi cha The Play List cha Times FM na mitandaoni. Katika maelezo yake Mwakyembe amesema inaelekea sasa Diamond ameanza kulewa umaarufu sasa. Kuhusu hoja ya vikao anavyodai mwanamuziki huyo Mwakyembe amesema kuwa “kama ni vikao na wasanii, tumefanya vingi sana, lakini Diamond hahudhurii vikao hivyo na si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao chake mwenyewe, haijalishi nibmaarufu kiasi gani." "Hatuwezi kuwa na sheria kwa wasanii wengine na sheria maalum kwake, nadhani hizi ni dalili za kuanza kulewa umaarufu kwani Diamond si Kiongozi wa Shirikisho la Muziki wala msemaji wa Chama cha Muziki wa kizazi kipya kuwasemea wenzake," amesema Mwakyembe. Aidha Waziri Mwakuembe amemalizia kwa kumshauri mwanamuziki huyo kuwa "si busara kwak...