ZANZIBARI YENYE KUPENDEZA.

NZANZIBARI YENYE KUPENDEZA.
"ZANZIBAR" Jina hili linaasili ya kiarabu au kiajemi
Wajemi wao kwao upande wao wamelitohoa neno hili katika neno "Zang bar" ambalo lina asili ya neno "Zinj" nyeusi, hivyo walimaanisha mwambao wa watu weusi, Waarabu wao wamelitohoa kwa neno "Zayyin dhal bar" yaani "mzuri mwambao huo"
Jina ambalo lilithibitishwa na Norman Benett, alipokuwa katika msafara wake ndani ya mwambao wa Africa Mashariki mwanzoni mwa karne ya ishirini, alijikuta akitamka maneno yafuatayo mara tuu baada ya kukiona kisiwa cha Zanzibar.
"Kwayakini hakuna kitu chochote kilicho kizuri kama Zanzibar "
Wanzanzibar wanamsemo wao walioutoa kwa Siti binti Sadi unaosema" Zanzibar ni njema atakae aje "
kadhalika muimbaji anasema" Nasikia ni kizuri tena kinanukia marashi ya karafuu".
Aidha mwimbo mwingine unabainisha zaidi kwa kusema.

"Kijogolo sina nyumba najenga barabarani, nitajenga nyumba ya mawe gorofa nje kwa ndani, sijaona manuari kupita barabarani, kama huamini nenda Mombasa au Unguja".
Utukufu wa Zanzibar si tuu kutokana na uzuri wa mandhari yake bali Zanzibar imepata utukufu huo kutokana na ujio wa misafara ya watu waliotukuzwa na Mwenyezi Mungu pamoja na Sharifu zao kuweka taasira kubwa ya maisha ya wanzanzibar kuwa katika ustaarabu wa hali ya juu yanatokana na mafundisho matukufu.

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!