NGUVU ILIYOPO KATIKA MANENO


NGUVU ILIYOPO KATIKA MANENO ~The Blessed




Maneno kwa lugha rahisi ni matamshi au maandiko au sauti au video inayoelezea akili/moyo wa mtu ulivyo.:Maneno unayoongea,maana yake ndiyo akili yako,na ndiyo yaliyojaa moyoni mwako.(luka 6;45).

Maneno yako ndio nia yako uliyo nayo moyoni.Maneno yako ndio maisha ya.Maneno yako,ndivyo ulivyo ndani na nje.UNACHOONGEA NDICHO UNACHOWAZA,NA NDICHO UNACHOKIAMINI,NA NDICHO UNACHOKIISHI AU UTAKAACHO KIISHI.
USIPOFUNGUA KINYWA CHAKO UKAONGEA,AU UKAANDIKA,HAKUNA ATAKAEJUA UNACHOWAZA.Ndio maana katika interview kuna kuandika na kuzungumza.Hata kama una akili kiasi gani,lazima uzungumze ili watu wakuelewe na wakujue ulivyo.

Na ndio maana nchi nyingi wakati wa uchaguzi wagombea wanazunguka kuzungumza na wananchi na kutoa ya moyoni.wanazungumza na kupewa maksi aidha wanafaa au hawafai kuchaguliwa.

 What is POWER??Nguvu maana yake ni ule uwezo wa kufanya jambo baya au zuri.POWER is the ability either to push or pull.Kuna nguvu gani katika maneno tunayotamka au kutamkiwa??

JINSI ULIVYO NI MATOKEO YA MANENO ULIYOJINENEA WEWE MWENYEWE AU ULIYONENEWA.
KAMA UKO VIZURI NI MATOKEA YA MAMBO MAZURI ULIYONENEWA.NA KINYUME CHAKE.

Katika makuzi yako,umepitia mikononi mwa wazazi/walezi/walimu na jamii kwa ujumlaWAMEKUTAMKIA NINI?????WALIKUAMBIA WEWE NI NANI???MWALIMU WAKO SHULENI ALIKUAMBIA NINI???

Ulivyo sasa,ni matokeo ya maneno yaliyonenwa juu yako.Tusome neno kidogo tu.Mithali 18:21,Mauti na uzima,huwa katika uweza wa ULIMI(maneno).
Kama tuko pamoja nipungieKwa hiyo kufa au kuishi,ni mdomo wako.biashara yako kufa au kustawi,ni ulimi wako.Mauti sio lazima ufe kabisa kimwili,hata maisha yako)Tusome tena Mithali 6;2.

UMETEGWA NA KUKAMATWA NA MANENO YA KINYWA CHAKO.na mithali 12:14UTASHIBA MATUNDA YA KINYWA CHAKO.Tunajadili NGUVU ILIYOKO KATIKA MANENO.Haijalisha unajitamkia au umetamkiwa au unatamkia wengine.NGUVU NI ILEILE,maadam yametamkwa.

Katika maneno yetu ya kila siku ziko nguvu kuu mbili.na huwezi kuishi nje ya unachotamka.Kwa sababu unachotamka hakitoki hapo mdomoni.kimeanzi huko moyoni.na MOYONI  ndiko ghala kuu la maneno na matendo.Akili haifanyi kazi kabla ya moyo kutoa go ahead.

Neno linasema,LINDA SANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO,MAANA NDIKO ZITOKAZO CHEMCHEM ZA UZIMA.NA AKASEMA,KIMTOKACHO MTU(MANENO)NDICHO KIUJAZACHO MOYO WAKO.

YAANI KWA MANENO YAKO,UTAKUFA AU UTAISHI,UTAKUWA TAJIRI AU MASIKINI,UTAAJIRI AU UTAAJIRIWAUTAOLEWA AU HUTAOLEWA.MANENO YAKO YANA NGUVU KULIKO INAVYOFIKIRI.

Tuanze mifano ya matamshi na matokeo yake.Muasisi wa nchi yetu ,alitamka kuwa Tanzania ni nchi ya aina gani????Wakati unaendelea kutafakari alichotamka muasisi wetu,kumbuka ukifuatilia wakati wa uumbaji wa MUNGU ,kila alichokiumba;biblia inasema,ALIONA NI CHEMA .Maana yake alitamkia mema uumbaji wake.
NI MARA NGAPI UMESIKIA MASIKIONI MWAKO VIONGOZI WENYE DHAMANA,WAKITAMKA MARA NYINGI SANA KUWA TANZANIA NI NCHI MASIKINI????

Kiongozi alipoingia madarakani,aliona (moyo)vitu vitatu.UJINGA,MARADHI NA UMASIKINI.Kinywa kikatamka.na taifa likatangaziwa.LAKINI HAKUONA UZURI WA NCHI YETUKAMA DHAHABU,MITO,MBUGA ZA WANYAMA.
Unataka kuniambia nchi ilijaa wajinga,magonjwa na masikini???hapakuwa na kizuri cha kumtukuza Mungu.Kwa hiyo  Mungu kuifanya Tanzania,work done was zero.kweli????

WAKATI WENZETU WAMEANDIKA KWENYE KWENYE HELA YAO MANENO YA KUMTUKUZA MUNGU KUWA "IN GOD WE TRUST"(kwa sababu fedha na dhahabu ni mali ya Bwana.)hayo ndiyo maneno yao.KWA NINI DOLA ISITAWALE DUNIA,WAKATI WAMEKIRI KWA VINYWA VYAO KUWA THEY TRUST IN GOD????

WAKATI WAO WANAKIRI HAYO,NA KUWEKA NYOTA KATIKA  BENDERA YAO,(nyota siku zote inangaa.hata Yesu alipofufuka,waliiona nyota yake mashariki).SISI TUMEKAZANA KUMSUTA MUNGU KUWA TANZANIA NI MASIKINI,PAMOJA NA UTAJIRI ALIOTUPA AMBAO HAUPO HATA KWA WENZETU.BENDERA YETU INA MPAKA BLACK COLOR. Na tulitamkiwa kuwa africa IS A DARK CONTINENT.unategemea nini??

Kwa maneno aliyotamka kiongozi mkubwa ardhi ikaandika,kwa nini tusivae chupi walizovaa wenzetu na kujiona ni sawa tu??Kila wakati tunasaidiwa na wenzetu.Marekani wao nani anawapa missaada.?? .

HAWAHITAJI MISAADA KWA MAANA UCHUMI WAO WAME UCONNECT NA MWENYE FEDHA NA DHAHABU.Nyinyi fedha yenu ikoje.???ndio kwanza ina picha za nyoka???.

TURUDI KWENYE MIFANO YA WATU BINAFSI.kila wakati hapa tunatoa mifano ya watu waliofanikiwa akiwemo NICK WA AUSTRALIA.Swali,huwa anajitamkia maneno gani?????ulishawahi kusoma mahali ameandika yeye ni kilema????? .Kijana yeyote aliyewahi kusoma mahali hao watu waliofanikiwa wakijitamkia kuwa wao ni masikini au vilema.waseme.

Kama ulishawahi kumsikia Reginald Mengi akisema yeye ni mfanyabiashara mdogomdogo niambie hapa leo.HUWA UNAJITAMKIA NINI??MAMA YAKO ALIKUTAMKIA NINI???MWALIMU WAKO ALIKUAMBIAJE???

KUMBUKA TU.MANENO YANA NGUVU.Umeshindwa kusonga mbele kwa sababu ya maneno uliyoaminishwa na unayoendelea kujitamkia.TANZANIA INA WASOMI WA KUTOSHA.TENA MAINJINIA .ni watanzania wangapi wanapewa tenda za kujenga barabara???Ni watanzania wangapi wanamiliki migodi???shida sio wao wala serikali.SHIDA WALITAMKIWA KUWA TANZANIA NI NCHI MASIKINI.

NCHI MAANA YAKE NI WATU.NCHI MASIKINI MAANA YAKE NI MKUSANYIKO WA WATU MASIKINI.NCHI TAJIRI MAANA YAKE NI MKUSANYIKO WA WATU MATAJIRI.NI NGUMU SANA KUONDOKA KWENYE MANENO YALIYOJENGA MSINGI WA MAISHA YAKO.

Kuna watu walitakiwa wawe madaktari,lakini wakakutana na walimu wasiojitambua wakawaambia masomo ya sayansi ni magumu hamuwezi (MANENO)na wakakata tamaa.KUMBUKA WALIOKUTIA MOYO(waliokutamkia maneno mazuri)na yakakuinua.

Walioko mahakamani,wanahukumiwa kwa maneno yaliyotungwa(vifungu vya sheria)yawe mabaya au mazuri.Nchi inaongozwa na katiba(maneno yaliyoandikwa ).Ndio maana kuna wakati wananchi wanataka katiba ibadilishwe(maneno /matamshi)
Nenda kariakoo.wale wafanyabiashara wakihojiwa na vyombo vya habari wanasema.Serikali itusaidie sisi watu wa hali ya chini..Au serikali ituangalie sisi wafanyabiashara wadogowadogo.Hawatainuka hapo.watauza malimao hata miaka hamsini.kwa sababu wameshajitamkia hivyo.

Kwa nini watanzania wengi wanajitamkia hivyo???NI KWA SABABU NDIO ROHO ILIYOWEKA MISINGI YA NCHI.Mtoto akizaliwa Tanzania,anaenda shule anaambiwa lengo la elimu ya msingi ni kupambana na maadu watatu.maradhi ,ujinga na umasikini.

Tuende sehemu ya mwisho ya nini cha kufanya ili tutoke hapo
Vijana wengi sikiliza salamu zao.wanasalimianaje?????wanaitana majina gani????Vijana wakikutana utasikia,Niaje mchizi wangu.Mambo niaje,Kijana mwingine anajibu,Mzuka tuu!Mzuka maana yake nini??Mchizi maana yake nini???
Haya maneno vijana wanayojitamkia kwa kujidai ni salaam za kisasa,yamewafanya kuwa machizi kweli.Huwezi kuvaa suruali ukaonyesha chupi yako nusu kama sio chizi(maneno uliyojitamkia)Huwezi kukaa kijiweni masaa nane ukizungumzia mafanikio ya Lionel mesi na kujua kila mchezaji wa nje analipwa nini,wakati wewe una miaka 27 unakaa kwa shemeji yako.

 MANENO YAKO YAKO NGUVU.NGUVU MBAYA AU NZURI.NI UAMUZI WAKO

Wakati Tanzania hata ambao wamepoteza mkono mmoja tu ,wanajiita ombaomba na wanakaa mpaka nje ya ikulu,Nick aliamua lile neno Disable akalibadilisha kuwa God is able,UNAJITAMKIA MANENO GANI?UNAMTAMKIA MUMEO/MKEO MANENO GANI??WATOTO WAKO UNAWATAMKIA NINI???

Unawaambia watoto wako nini kuhusu elimu??uchumi??ndoa???n.k.Watoto watayaishi maneno ya baba na mama yao.haijalishi ni mabaya au mazuri.Kama wewe na mkeo mnawasema watu mbele ya watoto,wakikutana nae njiani,watamdharau maana wanakuamini wewe mzazi na unachosema.

CHUNGA MANENO YA KINYWA CHAKO.Ni Mara ngapi umesema HUWEZI.bila hata kujaribu hiyo kazi/biashara??MARA NGAPI UMESEMA SIKU HIZI HAKUNA WANAUME WAAMINIFU.mmeo akitoka nje ya ndoa unalia nini???.BAADHI YA WALIMU PIA NI KUNDI LINHINE LENYE MANENO MABAYA NA KUWAVUNJA MOYO WATOTO.

UKIMWAMBIA MTOTO HUWEZI,LILE NENO LINAMKAA MAISHANI MWAKE.NDIO MAANA HATA WEWE UNAKUMBUKA MAMBO MENGI ULIYOAMBIWA UKIWA NA UMRI KUANZIA MIAKA MITATU HADI KUMI NA MBILI AU KABLA YA BALEHE.

CHUNGA MANENO YAKO.YANAWEKA MSINGI WA WATOTO WAKO.
UKIMWAMBIA MTU,NITAKUPIGA AU NITAKUUA Utafungwa maana maneno mabaya yanaumiza sana sana.UKIMWAMBIA MTU NAKUPENDA SIPATI USINGIZI KABISA NIKINYWA MAJI NAKUONA KWENYE GLASI.Haya maneno ni mazuri sana.yanasuuza moyo.hata kama hakuwa na mpango na wewe atakubali,akija kujuta ni baadae.

MAUTI NA UZIMA,VI KATIKA UWEZA WA ULIMI.Basi sisi tutumie  ndimi zetu positively.(kunena mema)YAANI HII IANZE NA MTU MMOJA MMOJA,BAADAE FAMILIA,BAADAE JAMII NA HATIMAE TAIFA.tukiendelea hivyo,baadhi ya watu wameshaanza maombi ya kufuta haya maneno.

[Halafu tuwe na nidhamu ya kinywa .Ukiamka asubuhi,sema hivi,ee Mungu,weka mlinzi kinywani mwangu.(zaburi 141:3)Huyu mlinzi ambae ni Roho mtakatifu.atakuchagulia maneno ya kuongea.Hutaongea kila neno.Maneno ni sumu Na maneno ni asali pia.

Kuna watu wamefungwa kwa maneno tu.Kuna watu wamevunja ndoa kwa maneno tu.Kuna watu wamefukuzwa kazi kwa maneno tu na umbea.Kuna watu wamelaaniwa na wazazi wao kwa ajili ya maneno yao.Kuna familia zimesambaratika kwa sababu ya maneno.

Unatamka nini???unanena nini??Maneno yako ndio maisha yako.HATA MWIMBAJI MMOJA AKAIMBA VILE UNAVYOKIRI ,NDIVYO UTAKAVYOKUWA.Ni maneno matamu tu ulimwambia mkeo ,mwenyewe akalainika akabeba begi akahama kwao akahamia kwako.NGUVU YA MANENO.

NI MANENO YA UONGO ulimwambia huyo mwanafunzi mpaka akaacha masomo akidhani utamuoa.hujamuoa.MANENO YA UONGO .(mithali 10:8) mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.UNATAMKA MANENO GANI??
maneno yako yanajenga au yanabomoa, Yanafarakanisha au yanapatanisha.
Yanainua au yanaua nafsi za wengine, Yote uliyojinenea umeyaona mwenyewe.
PALE ULIPOSEMA HUWEZI KWELI HUKUWEZAPALE ULIPOSEMA UNAWEZA,UMEWEZA.

Popote ulipo,unapoona pana kitu kisichofaa,Tamka unachotaka kiwe.Ayubu 22:23..inasema,utakusudia neno,nalo litathibitika.Tamka unataka watoto wako waweje.Ita watoto wako majina yenye utukufu.Adam alipomtazama Hawa alisema hii ni nyama katika nyama yangu,mfupa katika mifupa yangu.Wewe unasema,huyu mchaga sijui nilikutana nae wapi.Ita watoto majina yao mazuri.
Waite mainjinia,madaktari,pilot,walimu,wachungaji,wakue wakijua hivyo vitu vipo.

HATA UKIJIITA MASIKINI JANUARI MPAKA DISEMBA HAIKUSAIDII.UNAJIWEKEA MIHURI BURE.HAIKUONDOI HAPO ULIPO
JITAHIDI KUONA KITU KIZURI KWA KILA MTU AU KWENYE KITU UNAVHOKITAZAMA.ITAKUSAIDIA SANA.


Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!