HAYA NDIYO MASOKO YA UYOGA TANZANIA



HAYA NDIYO MASOKO YA UYOGA TANZANIA


Tumekuwa tukiulizwa na watu wengi sana juu ya soko la uyoga nchini Tanzania. Makala hii inajikita kuelezea hali halisi ya soko la uyoga na biashara kwa ujumla.
Uyoga na mazao yake (bahati mbaya hadi sasa tunazalisha uyoga pekee)  licha ya kuwa na faida kubwa kwa nchi na kwa kipato cha mwanachi mmomoja.Kilimo na  biashara ya uyoga katika nchi zinazoendelea kama Tanzania bado ipo chini sana. Kilimo kinafanyika kwa uchahe sana na kiasi kidogo; kwa maana ya kilimo kinafanyika si kibiashara hivyo kutokuleta tija kwa taifa na kwa wakulima.

Soko la uyoga
Je, Uyoga una soko?    Kilimo cha Uyoga kinalipa?
Awali ya yote bidhaa yoyote ili iweze kupata soko, ari, bidii na juhudi kubwa inabidi kufanyika kuanzia katika kuizalisha ili iwe  bora na inayopendwa na wateja;  pia katika kuitengenezea mazingira mazuri ya ya bidhaa hiyo kununulika kama  kuitangaza n.k

Tunasema uyoga una soko kubwa hasa hapa nchini na ni biashara kubwa. Zifuatazo ni hoja kadhaa zinazothibitisha hoja hii.

·     1. Uyoga ni utamaduni wa Mtanzania: Uyoga tangu enzi umekuwa ukitumika kama chakula na dawa kwenye makabila mengi hapa nchini Tanzania. Makabila mengi kipindi cha masika wamekuwa wakivuna uyoga porini  na kuutumia kama mboga au kutibu magonjwa mbalimbali; pia uyoga hukaushwa na kutunzwa kwa matumizi ya baadae. Uvunaji au ukusanyaji wa uyoga huu hukabiliwa na changamoto kadhaa kama; 

(a)  uyoga hupatikana kipindi cha mvua (masika) pekee
(b)  kushambuliwa kwa wavunaji na wadudu au wanyama wakali kama nyoka n.k,
(c)  kuvuna/kukusanya uyoga wenye sumu kimakosa (kuna uyoga unaofaa kuliwa na wenye sumu ambao haufai kuliwa na mwanadamu).
(d)  uharibifu wa mazingira; kuna mahusiano makubwa baina ya uyoga na mazingira endapo; mazingira hayatatunzwa ipasavyo uyoga hautamea/hautapatikana. Hivi sasa uyoga haupatikani kwa wingi kutokana na uchafuzi wa mazingira.
Hii hoja inadhihirisha kuwa kilimo cha uyoga ni fursa kubwa nchini, uwepo wa teknolojia ya kulima Uyoga inafanya Uyoga upatikane kipindi chote cha mwaka (na kama tafiti zikifanyika kwa wingi aina nyingi za uyoga kutoka porini zitalimwa kwenye mashamba ya uyoga), kupunguza vifo vitokanavyo na ulaji wa uyoga sumu au kushambuliwa na wanyama, na pia kusaidia utunzaji wa mazingira. Endapo wakulima watalima uyoga kibiashara; uyoga ni biashara kubwa na itawezesha kuongeza pato la taifa na kuwa chanzo cha ajira nchini.

2  2. Kubadilika kwa mtindo wa maisha  : kumekuwa na uhamiaji mkubwa wa watu kutoka vijijini kwenda mjini; hii imesababisha ile ari na mwamko wa ulaji wa uyoga kupungua kwani licha ya kuwa na mtu anauhitaji mkubwa kwani alikuwa anaula alipokuwa kijijini. Hii imesababishwa na kutopatikana kwa urahisi uyoga maeneo ya mijini, mtu akihitaji uyoga ni lazima aagize uyoga vijijini. Kutokana na mwamko wa ulaji wa uyoga kushuka imepelekea kizazi kinachofuatia pia kutokuwa na ari na mwamko wa kula uyoga licha ya faida zinazopatikana mwilini.
Mtindo wa maisha  ni pamoja na ulaji, ulaji kwa miaka ya hivi karibuni umebadilika kutokana na sababu mbalimbali  watu sasa wameacha au kupunguza  kula vyakula vya asili na kupendelea kula vyakula vya kisasa.

·      3. kuwepo kwa wageni kutoka nchi mbalimbali; baadhi ya nchi ulaji wa uyoga ni utamaduni unaoendelezwa, kutokana na faida za kilishe zinazopatikana kwenye uyoga, hivyo wanapokuwa hapa nchini hupendelea kuendelea na utamaduni wao. Kumekuwa na migahawa mingi nchini inayopika vyakula mahsusi kutokana na utamaduni wa taifa fulani, mfano migaawa ya kichina, kifaransa, kijerumani n.k
·          Uwepo wa mahoteli, migahawa (restaurants), maduka makubwa ya vyakula na vitu vingine (supermarkets); hoteli na maduka makubwa ni sehemu zenye uhitaji mkubwa wa bidhaa hasa za kilimo na Uyoga ukiwemo.

·       4. itaji mkubwa wa uyoga unaolimwa au kupatikana ukanda wa afrika; mataifa mbalimbali ya ulaya yanaamini nchi zinazoendelea hasa za afrika bado mazingira hayajachafuliwa sana kulinganisha na nchi zao. Hivyo mataifa hayo hupendelea bidhaa nyingi hasa za kilimo ukiwemo uyoga kutoka ukanda wetu wan chi za kiafrika; ingawa bado uyoga haujapewa kipaumbele kama mazao mengine ya kilimo.

·      5. wamko mdogo wa kulima uyoga: Nchini Tanzania na nchi zingine za kiafrika kilimo cha uyoga bado hakijatiliwa mkazo licha ya kuwa ni na faida kubwa kiafya, kiuchumi na kimazingira. Ni wakulima wachache sana wanaojihusisha na kilimo cha Uyoga kibiashara licha ya uhitaji mkubwa wa uyoga.
·       6. Kutokana na mabadiliko ya mitindo ya maisha hasa ulaji mbaya wa chakula kumekuwepo na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukizwa kama kisukari, shinikizo la moyo, matatizo ya figo n.k; wagonjwa wenye magonjwa hushauriwa kula uyoga. Pia kumekuwepo na mwamko mkubwa wa jamii juu ya ulaji wa vyakula vya asili (organic food) ikiwemo Uyoga hivyo ulaji na mahitaji ya Uyoga yanaongezeka siku hadi siku.
 
Mwisho:Kutokana na sababu tajwa na sababu nyingine nyingi tunathubutu kusema kuwa uyoga una soko kubwa na ni fursa mpya na yenye uwezo wa kuleta kipato kwa mkulima au mfanyabiashara wa uyoga na bidhaa zake na cha zaidi kuliingizia taifa pato kubwa. Ni sekta kubwa inayokuwa kwa kasi na endapo watanzania tutachangamkia fursa hii kwanza tutaimarisha afya za wananchi na kukuza uchumi wa nchi.

Comments

  1. tunaomba mifano ya makampuni labda au tunawezaje kuuza ma hotelini yaani connections za masoko atleast tupate motivation na sio report ya maelezo tu kwa mfano wenzetu Kenya wana kitu kina itwa FARM BIZ AFRICA wana chama cha uyoga ukiwa member unakua na nafasi ya kuuza zao lako, maelezo mazuri lakini yaambatane basi hata na makampuni yanayo nunua zao hilo.

    ReplyDelete
  2. Ni vyema kutambua mwandishi halisi wa makala. umecopy makala ya mtu mwingine (Hertu Mushrooms) bila ya kutambua sio fair kabisa kimaadili ya uandishi

    ReplyDelete
  3. Kichwa cha habari hakiendani na content. Umetuvuruga tu.

    ReplyDelete
  4. Taja masoko yako wapi acha blabla

    ReplyDelete
  5. Humu ndani mm ni mgeni, na ninapenda sana kulima uyoga baada ya kupitia mashamba ya uyoga
    Naomba mnijuze namna gani nitapata soko tafadhali ndugu zangu

    ReplyDelete
  6. Nitapata wapi soko la uyoga ,0747514474

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!