JINSI YA KUJENGA MVUTO WA SOKO
JINSI YA KUJENGA MVUTO WA SOKO
CHANGAMOTO YA MASOKO NA JINSI YA KUJENGA MVUTO WA SOKO
Ngoma kabwe
Watu wengi wanalalamika kuwa hawana masoko ya bidhaa zao na hiki kimekuwa kilio cha watu Wengi sana.Changamoto ya Masoko imewafanya watu wakate tamaa na biashara au ujasiriamali.Soko siyo changamoto kama wengi wanavyotazama.
Hakuna chakula kisichokuwa na soko au walaji. Wakulima wa Tanzania wanalima na wanafuga lakini hawana Masoko ati wakati pale Congo, Comoro, Sudani,Somalia wanahtaji vyakula kwa wingi.
Leo naomba niwambie kinachosababisha changamoto ya MASOKO NCHINI.
1.UBINAFSI(UMIMI)
2.UKOSEFU WA NIDHAMU YA KUHUDUMIA SOKO
3.KUTOJIAMINI
4.UKOSEFU WA TAARIFA SAHIHI
5.UZALISHAJI HAFIFU
1.UBINAFSI
Hii ni sababu kuu inayopelekea kuwepo kwa changamoto ya Masoko.
Wajasiriamali wengi wana ubinafsi yaan MTU anajua soko lakini hana uwezo wa kulihudumia lakini hawezi kumwambia Mwenzie,
Katika tafiti Tanzania tumegundua kuna masoko Mengi ambayo yanahtaji supply lakini bahati mbaya Watanzania hawana uwezo wa Kusuplly soko kutokana na kwamba uwezo wa Uzalishaji ni mdogo kwani kila mtu anazalisha kivyake na kibinafsi.
Watanzania wajasiriamali wanaogopa kuonyeshana fursa za Masoko kisa yeye atakosa wateja. Hata kama soko linamzidi uwezo uwezo yeye Hawezi kumshirikisha mwenzie Bali atakaa anamzungusha mtejaa na baadae mteja anamwona mbabahishaji anamkimbia.
Mfano mtu anapata tenda supermarket wakati labda uwezo bado haujawa wa kutosha. Atapeleka wiki moja afu anaishiwa mzigo, sasa badala ya kumshilikisha mwenzie mkulima au mfugaji yeye ataanza Udalali na badae kuchakachua .Na hapo mteja akijua anafuta tenda yako.
Wakati ungepata Tenda ukawashirikisha wenzio mkajiunga kikundi au umoja wa kuhudumia solo basi mngefika mbali. Ila coz ya Ubinafsi wenzako watakosa soko na wewe utakosa soko. Ndo maana leo Tunalia na Masoko.
2.UKOSEFU WA NIDHAMU YA KUHUDUMIA SOKO.
Katika anga za Kimataifa na anga LA kitaifa watu wengi hawapendi kufanya biashara na Watanzania cozi wanasema Watanzania ni wasumbufu kwenye biashara.Yaani MTU anapewa tender, kuwa alete mzigo mda fulani, kiasi Fulani na kwa ubora Fulani yeye anafanya kinyume. Umemwambia alete mzigo saaa tatu asubuh atakuletea SAA Tisa na SABABU lukuki au analeta kesho yake.Hapo samahan za kutosha.Na mwingine unamwambia lete kiasi fulan mfano trei 1000 anasema sawa naleta akifikisha mzigo anakuonyesha trei 50 na sababu Kibaooo.Unajielewa kweli?? kwa nini hukumwambia hiyo tenda huiwezi na umwambie uwezo wa oda yako ??.
Huyu ndiye balaa sasa yeye anajiita Mbongo orijino au mjanja. Anaambiwa alete tani moja yeye kila gunia anapunguza kilo moja akijua si watashusha na kuweka chini kumbe jamaa wanapima kila gunia bana. Sasa wanamaliza kupima wanagundua kilo kibao hazipo kweli unajielewa wewe unachokifanya.
Hiyo yote ni Kukosa nidhamu ya Kuhudumia soko. Alafu tukikosa soko tunalalama MASOKO HAYAPOOO .Toka Lini chakula kikakosa soko au walaji wewe .Nidhamu mbaya ya kuhudumia solo imewafanya Wakenya, WAARABU NA WAHINDI wachukue SOKO LETU SISI uku tunalia na soko.Kama unataka soko JENGA NIDHAMU NZURI YA KUHUDUMIA SOKO.
3. KUTOJIAMINI.
Wajasiriamali wengi wa Tanzania hawajiamini.Yaan MTU bidhaa ni yake lakini hana uwezo wa kuielezea vizuri au kuiuza sokoni afu anasema SOKO HAKUNA.
Unakuta MTU anauza kitu cha kawaida sana lakini bwana anavyojieleza na kueleza bidhaa yake ni kama hajawah nunua akatumia.
Mfano Mimi nafundisha na kuhamasisha ufugaji Mende kibiashara ila nikikuuzia wazo hili utalinunua tu. Juzi saba saba nimemuuzia wazo hili Mtanzania mmoja mwenye dola zake yaani ata leo anataka anipe milioni 10 tufanye huu mradi.Wewe una tikiti, tango, nyanya ambazo Wabongo wanakula alafu unasema Huna SOKOOOO.Mimi MENDE nauza we nyanya huna soko.Kama huamini niletee Mende kg 1 nikuuzie tena kwa Mtanzania.
4.BIDHAAA HAFIFU.
Wajasiriamali wengi nchini wana bidha zisizokuwa na ubora. Wengi wanazalisha bidhaa pasipo kuwa na hata MAARIFA kidogo ya kuzalisha bidha.Mfano MTU anafuga kuku wa Nyama walioletwa wakiwa na umri mmoja na kg sawa lakini wakati wa kuuza Mara huyu ana uzito robo, yule nusu na yule kg 1. Yaani haileweki.Lakini kwa mjasiriamali anayejielewe utakuta kukua wana umbo sawa, Uzito saws na bei sawa.
Sasa unakuta Mtu anaenda Nakumati kutafuta Soko alafu anaambiwa leta sampo, kwanza anataka sampo yenyewe alipwe.Sampo hiyo sasa kuku huyu robo yule nusu yule nusu ya robo.halafu eti huyu anatafuta SOKO .Nani atakupa soko lake??
Wateja wanataka bidhaa zenye ubora na zenye viwango. Yaan paja LA kuku huyu na huyu vifanane. Ukiambiwa lete kuku wa kg 2 wooote wawe kilo 2. Weka package nzuri.Maana wengine wanajifanya wachaga sana. Eti anaweka KIFUNGASHIO cha kawaida ila asipunguze faida kumbe ndo anajifukuza sokoni.
WAPENDWA MKITAKA MASOKO YAPO MENGI TU SEMA HAMYAONI KWA KUWA MNAPINGANA NA MAHITAJI YA SOKO
Hii imewafanya Wakenya, Wanyarwanda, Wamalawi,Wasouth Africa kulifaidi SOKO letu wakati sisi tunalia na Masoko.Ukitaka soko TENGENEZA MVUTO WA SOKO BWANA🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓
JINSI YA KUTENGENESLZA MVUTO WA SOKO.
Mvuto wa soko ndio unamfanya mteja aje kununua kwako na si kwa mwingine.
Huitaji kuangaika au kulilia SOKO. SOKO LIPO NA LITAENDELEA KUWEPO MILELE.
WEWE hangaika sana kutengeneza Mvuto wa Soko.Na hii ndo MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANI tunashughulika nacho Kwa wanachama wetu haswaaa yaani KUWATENGENEZEA MVUTO WA SOKO. ndo maana uku ukiwa na MENDE, soko unapata FUNZA soko unapata,UYOGA soko unapata,MCHAICHAI soko unapata na ndo maana tunasema HAPA CHANYA TUUU.HIVYO ukitaka MASOKO WEWE weka nguvu kubwa katika Kujenga mvuto wa Soko LA bidhaa zako.
JINSI YA KUJENGA MVUTO WA SOKO.
- Jenga NGUVU ya kuhudumia soko kwa Umoja ili kuondoa Ubinafsi.
- JENGA KUJIAMINI
- STAWISHA UBORA WA BIDHAA YAKO AU ONGEZA THAMANI KWA BIDHAA ZAKO.
- JENGA NIDHAMU THABITI YA KUHESHIMU NA KUTHAMINI SOKO.
- Jamani Masoko ni makubwa sana ni sisi kujiweka vyema ili tuingie katika mfumo rasmi wa Biashara au ujasiriamali.
.
Comments
Post a Comment