Wastara agundulika na tatizo jingine

Msanii wa filamu za Bongo, Wastara Juma amerejea nchini toka India alipokuwa ameenda baada ya kupata fedha alizochangiwa na Rais, John Pombe Magufuli na wananchi za kumsaidia kupata matibabu ya mguu na mgongo ambavyo vilikuwa vinamsumbua kwa muda mrefu.
Wastara amefanya mahojiano na vyombo vya habari mara tu baada ya kurejea nchini ambapo ametoa ripoti fupi kuhusiana na yaliyojiri huko India alipokuwa akifanyiwa matibabu.
Ameeleza kuwa amefanyiwa vipimo vyote na kugundulika kuwa ana tatizo kwenye fuvu la kichwa ambalo limeonekana kuwa na mpasuko kwa nje na kumsababishia uvimbe hali ambayo ilikuwa ikimpelekea kukosa usingizi. .
“Ni tatizo ambalo lilikuwa linahitajika kuchukuliwa umakini kwa sababu muda mwingi nilikuwa nalalamika kukosa usingizi, kitu ambacho mimi mwanzo nilikuwa nadhani labda ni kutokana na mawazo niliyokuwa nayo lakini siyo hivyo. Kwenye fuvu la kichwa kuna mpasuko kwa nje na kusababisha kama uvimbe jambo ambalo lilikuwa linanisababishia kukosa usingizi”, amesema Wastara.

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!