uKIMWI NA EBORA NI SIRAHA ZA MANGAMIZI Pt. 2


Karibu katika muendelezo wa makala yetu. Natuma wote niwaziwa wa Afya,namini utajifynza mengi.




Punde nitakuelezea ni kipi kinacho sababisha Ukimwi lakini siyo HIV.

Kwa mantiki hii kwa nini basi watu wapokee chanjo dhidi ya ukimwi? Nipeni sababu jamani. Mwili ambao mfumo wake wa ulinzi uko vyema unatengeneza askari wa kupambana na virusi wa aina mbalimbali ndani ya wiki tu. Sikiliza maneno ya Dr. Luc Montagnier, mshindi wa zawadi ya Nobeli, mkufunzi kwenye elimu ya virusi mbalimbali, anasema,
“Tunaweza kupokea virusi vya HIV mara nyingi bila kuathirika navyo. Mfumo wetu wa ulinzi ndani ya mwili unatengeneza askari seli wa kupambana na virusi hao ndani ya wiki chache, kama mfumo wako wa ulinzi ni bor.

Nadharia kuhusu ‘janga’  la ukimwi namna lilivyo anza na linavyo endelea kutafuna maisha ya watu, ina mapungufu mengi achilia mbali kuchukuliwa kama ndiyo ukweli wa msingi na serikali nyingi duniani pamoja na taasisi zake. Katika ulimwengu huru wa sayansi na tiba nadharia hii ya ‘janga’ la ukimwi si sahihi na wala haifai kuchukuliwa kama ukweli wa msingi kwa sababu nadharia hii haijaweza kukidhi vigezo vya kisayansi vinavyo hitajika kuifanya kukubalika kwenye ulimwengu huo kama ndiyo ukweli wa msingi juu ya suala zima la virusi vya HIV na ukimwi.

Vigezo vinavyo kubalika kisayansi katika ulimwengu wa tiba ni ‘Kanuni Koch’, kanuni hii ilitambulishwa karne iliyopita na bwana Robert Koch ambaye mwaka 1882 aligundua kirusi kisababishacho kifua kikuu, mwaka 1883 aligundua kirusi kisababishacho kipindupindu, na mwaka 1905 alipokea tuzo ya Nobeli kwa upande wa tiba. Kanuni ya Koch inatumika kama kanuni ya msingi katika kutambua kama ugonjwa unaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine na kama ugonjwa huo unasababishwa na aina fulani ya kirusi. 

Lakini mwana baiolojia kutoka chuo cha Havard kwenye fani ya molekuli bwana Walter Gilbert anasema nadharia ya HIV kama ugonjwa unasababishwa na virusi na wakuambukizwa ina pingana na kanuni ya Koch.( Peter H. Duesberg & Bryan J. Ellison - IS THE AIDS VIRUS A SCIENCE FICTION?, IMMUNOSUPPRESSIVE BEHAVIOR, NOT HIV, MAY BE THE CAUSE OF AIDS, , Policy Review Summer 1990

Kanuni ya kwanza ya Koch: Kirusi lazima kipatikane katika seli zilizo athiriwa na ugonjwa. Lakini hakuna kirusi cha HIV unacho weza kukipata kwa karibu asilimia 10 mpaka 20 ya wagonjwa wa ukimwi. Mpaka hivi karibuni kwa kutumia vyombo vya kisasa zaidi katika vipimo, hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kirusi cha HIV na waathirika wengi wa ukimwi, yaani kirusi hicho hakipatikani katika seli ya idadi kubwa ya wagonjwa wa ukimwi moja kwa moja.( Ibid


Kanuni ya pili ya Koch:Kirusi lazima kiweze kujitenga na kirusi kingine kilicho tofauti na hicho na kiweze kujitenga na seli yenyewe au mwili wa mgonjwa. Hata hivyo kiasi cha virusi vya HIV kwa mgonjwa wa ukimwi ni kidogo sana kiasi kwamba virusi hivyo haviwezi vikajitenga au kutenganishwa moja kwa moja kutoka kwenye seli za mgonjwa. Njia pekee inayotumika ya kuweza kuvitenganisha virusi hivi na seli za mgonjwa wa ukimwi na mgonjwa mwenyewe ni kwakuchukua kiasi kikubwa cha seli kutoka kwa mgonjwa na kasha kuzitia seli hizo aina fulani wa mchanganyiko wa kikemikali ili kuweza kuvifufua virusi vya HIV na viweze kuonekana. Hali hii ni tofauti sana na magonjwa mengine yasababishwa na virusi ambapo, kunakuwa na kiasi kikubwa cha virusi vilivyo hai vinavyo wezwa kutangwa moja kwa moja na damu au seli zilizo athirika za mgonjwa. Virusi hivyo hufikia idadi ya kutoka milioni moja mpaka bilioni moja kwenye ujazo wa mililita moja kwenye plazma ya damu ya mgonjwa. Lakini si kwa virusi vya HIV ambavyo kwa mgonjwa wa ukimwi havipatikani zaidi ya elfu moja kwa kila ujazo wa mililita moja wa plazma ya damu, tena kwa kutumia aina fulani ya kemikali kwa damu iliyo chukuliwa kwa vipimo, kemikali hiyo ndiyo itakayo muwezesha muuguzi kuviona au la virusi hivyo, na vinapo onekana pia idadi yake ni ndogo mno. Hapa utaona kabisa, kabisa HIV haiwezi kusababisha ukimwi.(ibid)



Kanuni ya tatu ya Koch:Kirusi lazima kisababishe ugonjwa kinapo ingizwa kwa mtu asiye na ugonjwa wa kirusi hicho. Kirusi cha HIV hakikuonesha kusababisha ugonjwa kilipoingizwa kwenye mwili wa nyani kwa majaribio wala kilipo ingizwa kwa wahudumu wa hospitali bila wao kujua. Endapo kanuni hii ya tatu kwa njia au sababu zozote zile itashindikana kutumika, basi mbadala wake lazima utumike, nao ni ushahidi wa kutosha kutoka kwa madaktari juu ya tiba kwa mgonjwa wa kirusi husika, mgonjwa anapaswa kupona na kirusi humalizwa nguvu kabisa baada ya kupokea tiba hiyo, lakini imekuwa ni tofauti hakuna chanjo wala dawa zozote dhidi ya HIV zilizo weza kuzuia au kutibu ugonjwa ukimwi, ingawa dawa na chanjo mpya zinapendekezwa kila uchao.(ibid)



Kanuni ya nne ya Koch:Kanuni hii inatumika pale tu kanuni iliyotangulia imetumika na kutoa majibu yaliyo tarajiwa au vinginevyo kanuni hii haina maana ya kutumika, na hapa hatuwezi kuitumia kwa vile kanuni iliyo tangulia haikutupa majibu tuliyo tarajia. Kanuni hii inasema kirusi lazima kwa mara nyingine baada ya mgonjwa kupona, kitenganishwe na seli iliyo athiriwa na ugonjwa mpya.(ibid)


HIV na kile kinacho daiwa kinatokana na virusi hao yaani ukimwi, kushindwa kuwiana na kanuni za Kochi kuna zua maswali mengine kama kweli ukimwi ni gonjwa la kuambukizwa. Kanuni za Kochi kwenye ulimwengu wa virusi na matibabu ni kanuni za msingi sana katika kuutambua ugonjwa, na ikiwa HIV na ukimwi zinakingana na kanuni hizi basi mbadala wa kimantiki inabidi utolewe na wale ambao wanao dai kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya HIV na ukimwi, mbadala ambao utakidhi haja tuliyoshindwa kuipata kwenye kanuni za Kochi kwa kufuata kanuni za sayansi ya virusi na kitabibu.

Mbadala uliotolewa na wale wanao dai kuwa HIV ndiyo inayosababisha ukimwi baada ya nadharia hiyo kushindwa kukubaliana na kanuni za msingi za kuweza kufahamu ugonjwa na tabia zake, kanuni za Kochi. Mbadala huo nao unakuja hivi ….

Beverly Griffin, mkurugenzi wa kitengo cha Virology katika Royal Postgraduate Medical School London anasema kuhusu mbadala huo. HIV imepewa Sifa zisizo zake ili kuweza kuunganisha virusi hao na maradhi ya ukimwi. Kikawaida virusi kama wa HIV inachukua takribani miaka kadhaa baina ya kipindi cha maambukizo mpaka kugundulika kwa ukimwi. Lakini ugonjwa unapo gundulika mwaka mmoja tu baada ya maambukizo ya virusi wa HIV, inakuwa ni vigumu kuwa na uhakika kama sababu nyingine hatarishi sizo zilizo sababisha ugonjwa (kama dawa zenye sumu kali na chanjo). (ibid)

Pili, kakuwa virusi wa HIV, kabisa hawapatikani katika kidondo, mkwaruzo au mchubuko wa mtu wenye virusi hao, wanasayansi wanatengeneza nadharia ambayo haina ukweli wa msingi kwamba ukigusana damu ya mwenye virusi ana asiye navyo basi asiye navyo naye atapata. Ingawa tumeshaona ni kiasi kidogo sana cha virusi hao wanapatikana kwenye damu ya mgonjwa na ambao inabidi kutiwa mchanganyiko maalum kuwafufua iliwaweze kuonekana kwenye vipimo vyetu. (ibid)


Tafsiri ya ukimwi nayo ni ngumu. Centers for Disease Control and Prevention (CDC) mwaka 1987 ilitaja maradhi 25, kama moja au zaidi ya maradhi haya yatapatikana kwa mgonjwa mwenye virusi vya HIV basi moja kwa moja mgonjwa atachukuliwa kuwa anayo ugonjwa wa ukimwi. Lakini moja ya maradhi hayo au zaidi endapo yatapatikana kwa mgonjwa bila virusi vya HIV, basi ugonjwa huo utatibiwa kama wenye, mathalani T.B ambao nao umetaja katika orodha ya magonjwa hayo 25. Lakini T.B inapopatika kwa mtu mwenye HIV moja kwa moja hatotibiwa T.B bali ukimwi, sasa hapa utajiuliza ukimwi ni nini?(ibid) 

Tatizo la Pili, sababu ya kukusanya magonjwa yote haya chini ya ukimwi ni kwa vile yote yanasababishwa na kitu kimoja, udhofu au upungufu wa kinga za mwili. Lakini hata hivyo upungufu wa kinga unashindwa kuowana na baadhi ya maradhi yaliyo orodheshwa na CDC, mathalani ugonjwa wa saratani na ugonjwa wa akili ambao nayo inapatikana kwenye orodha hiyo ya CDC.  
Tafiti zinaonesha kuwa saratani haiongezeki zaidi eti kwa vile mgonjwa anao upungufu wa kinga, na juu ya yote mfumo wa ulinzi unatumika kushambulia na kuulinda mwili na vitu vyenye madhara viingizwavyo ndani ya mwili, na seli za saratani ni sehemu ya mwili wa mgonjwa hivyo mfumo wa ulinzi hauwezi kuzishambulia seli hizo. Hivyo sababu iliyo tumika kuyakusanya magonjwa yote haya chini ya ukimwi haikidhi haja. (ibid) 


Ugumu  wa tatu  kwenye nadharia hii ya HIV kuweza kusababisha ukimwi ni udogo au uchache wa virusi vya ukimwi kwenye mgonjwa. Kwa kila T-Seli saidizi 10,000 ambazo zimeoneka kuathirika na ukimwi kunapatikana kirusi 1 au pungufu cha HIV. Ni vigumu kuelewa ni vipi virusi vya HIV vinaweza kuathiri mfumo wa ulinzi kwa kiasi cha kumsababishia muhusika ugonjwa wa ukimwi, ikiwa haviwezi kuathiri mfumo huo ila vijiseli vichache mno. Hata kama kila T-seli iliyo athiriwa na virusi vya HIV itakufa kasi cha T-seli zitakazo kufa hazitozidi kiasi cha T-Seli mtu yoyote anazo zipoteza endapo atajikata bahati mbaya wakati ananyoa au kwenye mchubuko kidogo tu. Upungufu kama huo mara moja unajaziwa bila hata kuuathiri mfumo wa ulinzi wa mwili kwa vile mwili wenyewe unazalisha T-seli kwa kiwango kikubwa zaidi kila wakati.(ibid) 

Ugumu wa nne ambao wana-virologist wameutaja kwenye nadharia hii ya virusi vya HIV kuweza kusababisha ukimwi ni kuwa; Virusi wa HIV wanapatika kwenye kundi la virusi wa aina ya Retroviruses ambalo ni kundi la virusi vilivyo na maumbile ya kawaida kulinganisha na virusi vingine, genetiki za virusi hivi ni chache mno. Makundi mengine ya virusi yanazo tabia ya kuuwa seli baada ya kuziambukiza na hivyo kusababisha ugonjwa, lakini virusi wa kundi hili la HIV na hapa nikimaanisha na virusi wa HIV wenyewe, huwa hawana tabia ya kuuwa seli, baada ya kuivamia seli virusi hawa wana kopi genetiki yao na kuitumbukiza ndani ya seli waliyo ishaumbulia, na baada ya hapo wanaiachia seli inaendelea kuishi na uhai wake unakuwa unategemea seli hiyo. Taratibu virusi hivyo vinaendelea kujizalisha kutoka kwenye seli waliyo iacha iendelee kuishi. Kwa hiyo aina hii ya virusi ni vigumu mno kuibambikiza kesi ya ukimwi ambapo sifa yake kubwa ni kufa kwa seli hai nyingi mno na kwa kasi sana kiasi cha mgonjwa kuwa na upungufu wa kinga. Lakini juu ya yote ni kuwa aina hii ya virusi kwenye idadi ya 50 mpaka 100 inapatikana imejificha kwenye DNA ya kila binaadam, na imekuwa ikirithishwa kutoka kizazi hadi kizazi tangu mwanzo mwa historia ya binaadam. Ni vipi leo hii aina hii ya virusi iweze kusababisha ukimwi?(ibid) 


sasa ni kipi kinachosababisha UKIMWI .... tukutane tena hapa next time ...

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!