Hali ya joto kanda ya pwani yazua gumzo
HALI YA JOTO: Wataalamu wamesema kuanzia wiki hii na kuendelea na zijazo kutakuwa na hali ya joto kubwa usiku na mchana katika Ukanda wa Pwani.
Joto hili linadaiwa linaweza kusababisha upungufu wa maji mwilini ambayo yanaweza kusababisha udhaifu mwilini, pia inaweza kufanya mtu apate ugonjwa wa chickenpox (tetemakuwanga), harara ama vipele vya joto mwilini pamoja na msongo wa mawazo.
Unashauriwa kunywa maji kwa wingi au vimiminika, kuoga mara kwa mara, kupunguza vyakula vya protein na badala yake kula zaidi mboga mboga na matunda kwa wingi. (Ni kutoka kwa washauri wa afya ya mwili).
Comments
Post a Comment