CHADEMA watoa tamko la kuhusu watu 40 waliokamatwa kwenye mandamano

Leo February 21, 2018, Chama cha Demokrasia na MaendeleoCHADEMA kimesema kitalishtaki Jeshi la Polisi na Serikali endapo watashindwa kutoa tamko kuhusu watu 40 waliokamatwa siku ya maandamano katika uchaguzi mdogo wa ubunge Kinondoni.
Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika amesema watu hao 40 walikamatwa February 16, 2018 wakati wakielekea Manispaa ya Kinondoni.
Mnyika amesema hadi sasa Jeshi la Polisi linawashikilia wananchi hao 40, ambapo kisheria lilipaswa kutoa haki kwa wananchi hao kupata dhamana.
“Tunalitaka jeshi la Polisi kupitia IGP kutoa kauli leo juu ya watu hao 40 wanaowashikilia na kuwaainisha kwa majina watu hao na kueleza taratibu za kuwapa dhamana ama iwapeleke Mahakamani.” – John Mnyika

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!