SERIKALI YA ISRAEL IMEAMUA KUWAWEKA JELA WAHAMIAJI WA KIAFRIKA WALIOKATAA KUONDOKA NCHINI HUMO,BAADA YA KUPEWA MUDA WA KUONDOKA NA KWENDA NCHI NYENGINE

SERIKALI YA ISRAEL IMEAMUA KUWAWEKA JELA WAHAMIAJI WA KIAFRIKA WALIOKATAA KUONDOKA NCHINI HUMO,BAADA YA KUPEWA MUDA WA KUONDOKA NA KWENDA NCHI NYENGINE

Mpango wa serikali unawapa watu wanaolengwa na hatua hiyo kuchagua kati ya kuondoka nchini Israel kwa "hiari" na kwenda nchi nyingine au kuzuiliwa jela kwa muda usiojuilikana.Siku ya Jumanne,Februari 20,kwa mara ya kwanza,wahamiaji saba waliokataa kuondoka nchini Israeli walifungwa.

Wahamiaji saba waliofungwa siku ya Jumanne walikuwa miongoni mwa watu 750 wanaozuiliwa wakati huu katika kituo cha Holot.Kituo hiki ambacho ni kama nusu jela kilifunguliwa katika jangwa la Negev,ili kuwaweka pamoja raia hao wa kigeni walioingia nchini Israeli kinyume cha sheria.Na serikali sasa inataka kufunga kituo hicho.

Raia hawa saba wa Eritrea walipokea wito kutoka kwa mamlaka ya Israeli mwezi Januari.Walipewa mwezi mmoja ili kuamua kati ya kuondoka "kwa hiari" na kwenda nchi nyingine au kuzuiliwa kwa muda usiojuilikana.siku ya Jumanne,watu hawa saba waliitwa na idara ya uhamiaji katika kituo cha Holot.Kwa mujibu wa mmoja wa wafungwa hao aliyehojiwa na TEAM SALUM ZANZIBAR,walitakiwa kutoa jibu lao.Raia hawa saba wa Eritrea walichagua kufungwa badala ya kuondoka nchini Israeli.

Mamlaka ya Israeli iliwahamishia katika gereza la Saharonim, zaidi ya kilomta mia moja kutoka Holot.Lakini wahamiaji hawa hawakuweza kuweka sawa nguo zao na vitu vingine.Hatua hii ya haraka inaonekana kama ukatili na wafungwa wa Holot. Kama ishara ya maandamano,wote waliamua kuanza mgomo wa kususia chakula tangu Jumanne usiku.

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!