Rais John Magufulu amezuia kuondolewa kwa kaya

IZO KAYA ZIACHENI HAPO HAPO''-MAGUFULI...soma zaidi
   
Rais John Magufuli amezuia kuondolewa kaya zaidi 1,900 zinazoishi katika nyumba zilizopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Mwanza hadi itakapofanyika tathmini kwa sababu wananchi hao ni wapigakura wake.
Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Februari 24, 2018 baada ya kuskiliza changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa uwanja huo ambao walimweleza kuwa uwepo wa kaya hizo unakwamisha ujenzi wa uwanja huo.
Akijibu jambo hilo,Rais amesemawasiondolewe hadi pale watakapolipwa madai yao huku pia akiwataka wananchi hao kutoendeleza makazi yao.
"Hawa watu ndio walionipa kura,pamoja na hivyo msiwaondoe hadi pale mtakapokamilisha kuwalipa madai yao," amesema Rais Magufuli.
Oktoba mwaka jana,Rais Magufuli aliagiza kusitishwa kwa ubomoaji wa nyumba za wananchi zaidi ya 2,000 wanaodaiwa kuvamia eneo la uwanja huo,kituo cha polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).


#http://ngomakabwe.blogspot.com/2018/02/mwandishi-wa-gazeti-la-habari-leo.html

Siku hiyo wakati akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa daraja la juu la waenda kwa miguu eneo la Furahisha jijini Mwanza,Rais Magufuli aliagiza ubomoaji huo usitishwe hadi atakapotolea uamuzi suala hilo.
Leo mjini Mwanza,Meneja wa uwanja huo, Ester Mandale alimweleza Rais kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa jengo la wasafiri,uwanja kukosa uzio pamoja na ndege kuzuiwa kubeba samaki.
Amesema baada ya ndege kuzuiwa kusafirisha samaki kwenda nchi za nje,wanalazimika kusafirisha kwa kutumia magari wakati wenzao wa Kenya wanatumia ndege,hivyo kuikosesha Serikali mapato.
Akizungumzia changamoto hiyo,Rais alimwagiza meneja huyo kufanya tathmini inayohitajika katika ujenzi wa jengo la usafiri pamoja na uzio kisha aiwasilishe kwa ajili ya kuanza ujenzi huo.
Kuhusu usafirishaji wa samaki,Rais Magufuli aliagiza kufanya uchunguzi kwa wenzao wa Kenya kujua  wanasafirishia kwa gharama kiasi gani.
Rais ameondoka jijini Mwanza na anaelekea Chato kwa ajili ya mapumziko.

Comments

Popular posts from this blog

DALA YA KISHETANI NA USHOGA EP. 5

JE WAJUA FAIDA YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO

PICHA ZA UCHI NI SHIDA KWA JOGOO WAKO!!!